Hana hamasa huyooo. Huyo mdada hana amsha amsha kama Manara .Ukweli ndiyo huo na msema kweli ni mpenzi wa Mungu tusijifariji kirahisi hivyo kuziba pengo la Bugati ni ngumu si rahisi kihivyo.Kama hamuamini tusubiri muda utasema
unaposema amsha amsha unaamaanisha kuongea vijembe na matusi au? maana Manara sikuona hizo amsha amsha miaka minne mitano nyuma akiwa pale simba..
team ikifanya vizuri haitaji propaganda na amsha amsha.. kila wiki watu wanajazana kwenye tv kuangalia team za ulaya.. zinapata pesa kwenye haki za matangazo ya tv sababu zina mashabaki dunia nzima
manchester hajachukua ubingwa miaka saba ila anakimbiza kwenye mapato ya television maana dunia nzima watu wanajazana vibanda umiza kuwaangalia..
ushaona wapi wanafanya amsha amsha dunian au hata kwao UK
mpira wa vijembe na matusi unatengeneza chuki.. ndo maana sasa hv simba na yanga chuki zimezid miongon mwa mashabiki sababu ya matusi..
90% ya mashabiki wa yanga wana chuki halisi na simba sababu ilikuwa manara..
ila simba hawana chuki na msemaji au mhamasishaji wa yanga sababu walikuwa hawatukani...
Haji angekuwa kama dismas ten wala yanga wasingeshangilia manara kuhamia yanga wangesema hawamtak ni simba damu ila sababu ya ile chuki walionayo wanashangilia wakijua sasa hv watakuwa wanatukanwa simba..
ingawa pia wanakwambia hawamuamini utaona kuwa hapo kilichowasukuma wamshangilie sio kuwa wanajua wa kwao hapana ni kuona sasa hv watakuwa wanashangilia matusi ya kwenda upande wa pili
its clear ndoa ya Yanga na Manara ni win win situation.. Manara pesa, Yanga mashabiki kushangilia matusi, Yanga gsm kupiga pesa ya ununuz wa jearsy manara akihamasisha mashabiki ila kwa afya ya Mpira hata pale Simba Manara alikuwa anatia doa Simba kwa baadhi ya matendo yake
nakwambia kama simba ingekuwa haifanyi vizuri Uongoz ndio ungeondolewa na Mashabiki akabak manara ila sababu Simba iko vizuri na Uongoz ukaona wanakoelekea Manara anakuwa anawaharibia wakat mwingine wakaamua wamminye kiutu uzima kulinda heshima yake
yeye akawa ana mawazo ya miaka ya 90 akijua wanachama wataandamana kina mo na Barbara watoke.. matokeo yake kasahau mpira wa Tanzania ushahama huko.. wanachama wa kufata mkumbo wamebaki wachache. mbaya zaid akawa hana support ya wale simba wenyewe kina magori na hans.. bora wale wangekuwa upande wake ingeweka uzito
sasa hv uwanjan shabiki wa simba kukaa upande wa yanga ni kosa la jinai.. inafikia hatua mashabiki wa simba wanaichujia Azam kisa Manara.. hii sio nzuri kibiashara..
jaman tubadilike kuendesha mipira kiswahili utatutia upofu wa kuona vitu vya msingi..
utan unaruhusiwa uwe na kipimo....