tenanzinyo
Member
- Dec 28, 2012
- 64
- 23
Habari wana jamii wenzangu!nimatumaini yangu kuwa wengi wenu mmekuwa mkikitazama kipindi maarufu sana cha MKASI kinachorushwa na na kituo cha runinga cha East Africa TV(chanel5) kikiongozwa na mtangazaji mahiri wa kike nchini salama jabiri!kiukweli maudhui ya kipindi ni mazuri sana hususani kwa sisi vijana kwani tunapata fursa adhimu ya kujua maisha ya watu mbalimbali maarufu hapa nchini hususan ktk tasnia ya siasa,michezo,filamu,muziki nk.niwape hongera wote waliobuni kipindi hiki.Tatizo langu mimi ni kuhusu matumizi ya lugha inayotumika wakati wa mahojiano kati ya salama na wageni wake,sometime inakera.ntatoa mfano mmoja wa hivi karibuni wakati anafanya kipindi na jackline wollper wakati majadiliano ya kiendelea alisikika akimwambia john" umedinda"nfkr ni baada ya john kumtazama sn Wollper mwanzoni nikajua labda amepitiwa ila wakarudia tena safari hii na muba na john wakalitamka hilo neno!Ashakum si matusi kwa mtazamo wangu kuna baadhi ya neno hili c matusi lkn ifahamike kwamba kipindi hiki kinatazamwa na watu wa rika tofauti tofauti kuanzia wototo wadogo mpk wazee!hebu upo imagin upo na mtoto wako unaangalia kipindi halafu akuulize hivi baba "kundinda"maana yake nini?cjui utamjibu nini?wito wangu kwa dada salama najua unauwezo mkubwa sana wa kuuliza maswali mazuri lkn kwa hili naomba ajitazame na kujirekebisha!ni mtazamo tu lakini wadau!