1. Kama kuna mchezo ambao Matola alipaswa kuonyesha umuhimu wake kuwa assistant coach ni leo..nadhani simba watafute ass. Coach mwingine, amechezea simba, amekuwa ass. Coach muda mrefu, lkn sifa hizo hazina mchango wowote kwa timu inapocheza mchezo km wa leo, sabab michezo inatofautiana, kitu cha kwanza kabisa ambacho simba players hawakuwa nacho ni winning spirit, walionekana wazi kabisa hata kwa kuwatizama kabla ya mchezo kuanza hawakuwa na spirit ya ushindi tofauti na yanga players..na Matola kwa uzoefu wake alipaswa kuwaandaa players kwa hili.
2. Simba inahitaji watu wenye maturity na football kwenye technical benchi, kujua kuongea sana na media au kufanya sijui uchambuzi hakumpi mtu maturity kwenye football na kuwa part ya technical bench..Ahmed Ally na wengine wawe replaced.
3. Simba watafute team captain mwingine, chuma s too junior kuwa kapten, ni jukumu zito kwake, kwa mfano kuna mara kadhaa maamuzi ya refa hayakuwa mazuri kwa simba, hayo tu yanatosha kuondoa attention ya mchezo kwa baadhi ya wachezaji..km alivyocheza zile rafu Inonga, siyo kawaida yake..kapten haongei na refa, haongei na wenzake ku-maintain attention muda mwingi yuko kimya, kwa wanaokumbuka lile goli simba walifungwa na Pirates halikuwa halali, kama kapteni alipaswa amfate refa kumwambia acheki VAR lakin alikuwa anazubaa tu..na simba walitolewa finally, wampe mchezaji mwingine senior player awe team kapteni.