Kumekuwa na hali fulani kwamba watu wakifanikiwa
kiuchumi au kusoma kidogo basi wengine wanasema
hakuna Mungu na kutaka logic kwenye kila jambo
linalohusu uwepo wa Mungu. Hawaamini hata immortality
life baada ya kufa.
Je nawauliza nyie ni zaidi ya Elon Musk ambaye ingawa haja
jishikiza kwenye dini ila anamini katika ukristo na uwepo wa
Mungu na kwa kipindi cha hivi karibuni amezidi kuamini sana.
Je ndugu zangu mnamkataa shetani na mambo yake na fahari
zake zote?
Kwanza kuna watu hawaamini Mungu kwa sababu wao ni masikini, hivyo hoja inayounganisha kutoamini Mungu na kufanikiwa kiuchumi haina mashiko.
Pili, kitu muhimu si kuamini. Kuamini ni haki ya kibinadamu ya kila mtu aamini anavyotaka. Imani inalindwa na haki ya kila mtu kuwa na faragha yake. Hii ni sehemu ya "Universal Declaration of Human Rights" tangu December 10, 1948. Ni kitu non negotiable hakihitaji mjadala wala justification. Amini unavyotaka. Usiingilie imani za wengine na uhuru wao. Ila imani ikiletwa public square kama hapa JF ni fair game tutaichambua.
Mimi sipo hapa kujadili imani ya mtu. Imani ni haki ya kibinadamu, kama ilivyo haki ya kutoamini.
Ndiyo maana kuna watu wana imani tofauti, maelfu ya dini, na wote wako sawa kuamini wanavyotaka. Hiyo ni haki yao.
Mimi niko hapa kujadili fact. Fact si haki ya binadamu kila mtu awe na yake. Fact ni objective.
Unaruhusiwa kuamini immortality na life after death. Mtu akikuingilia katika imani yako hiyo, hata mimi nitakutetea uamini unavyotaka, kwa sababu hiyo ni haki yako ya kibinadamu.
Ila, tukienda kwenye facts, immortality si fact. Hakuna evidence wala proof kwamba kuna maisha ya mtu yanaendelea baada ya mtu huyo kufa.
Swali la "nyie ni zaidi ya Elon Musk" ni logical fallacy ya argument from authority.
Kwa nini umemtaja Elon Musk? Kwani Elon Musk ana monopoly ya kuujua ukweli kuhusu uwepo wa Mungu?
Elon Musk hata si mwanatheolojia useme huyu anajua theolojia sana msikilizeni. Mimi nimebishana na Alvin Plantinga kwwnye masuala haya, na nikamshinda.
Sasa huyo Elon Musk unaweza kumlinganisha na Alvin Plantinga kwenye mambo ya theolojia?
Mbona unamuweka Elon Musk sehemu ambayo hana utaalamu nayo kwenye mambo ya theolojia? Hatushindani kuendesha kampuni ya roketi hapa, kwenye kuendesha kampuninya roketi ukitaka kunishindanisha na Elon Musk nitasema kanizidi uziefu huko, lakini kwenye faksafa ya dini Elon Musk ana credentials gani?
Pia, imani ni kitu very private and very complex.
Huyo Elon Musk unahakikishaje kweli anaamini Mungu yupo, na kwamba anapoonesha kuwa anaamini hivyo hafanyi hivyo kwa sababu inamsaidia kibiashara tu kupiga pesa, asiwaoneshe wateja wake kuwa yeye ni mtu ambaye hawatampenda? A lot of religion is virtue signaling, do you understand that?
Kama Mungu yupo, thibitisha yupo. Achana na logical fallacies za argument from authority za kumuangalia Elon Musk.
Elon Musk akila mavi na wewe utakula? Huoni kwamba unaweza kula mavi kwa kufikiri Elon Musk kala mavi, kumbe mwenzako kaitengeneza chocolate ionekane kama mavi.
Acha uvivu wa kufanya kitu kwa sababu Elon Musk kafanya, kwani wewe hunanuwezo wa kuchambua mambo ukajua mazuri au mabaya ni yapi?
Thibitisha Mungu yupo, acha longolingo za Elon Musk kimepanda kimeshuka.