Salamu na Shukrani toka kwa Maskini_Jeuri

Salamu na Shukrani toka kwa Maskini_Jeuri

Pole sana M_J....tunashukuru kusikia mengineyo yameisha salama
 
Wapendwa marafiki katika jina la Invizibo.

Kama mtakumbuka mwanachama hai wa MMU kitengo cha ISC ndugu yetu Maskini Jeuri alipata ajali mbaya sana takribani wiki tatu zilizopita.

Ilikuwa ajali mbaya iliyogharimu uhai wa binadamu mmoja, na wengine kujeruhiwa. Tunamshukuru Mungu, mpiganaji mwenzetu yuko salama na anaendelea vema.

Nimetoka kuongea naye hivi punde. Anawasalimu, Anawamisi na Anawashukuru kwa ushauri na pole mlizompa. Amefarijika sana. Ameniomba niwashukuru kwa niaba yake. Shukrani za kipekee kabisa amezituma kwa katibu Roya Roy. Mkuu unashukuriwa kwa msaada mkubwa uliompa. Ulimsaidia sana.

Pia kesi yake mahakamani imeshatolewa hukumu. Amepatikana na hatia katika makosa saba. Amepigwa faini ya Tsh 60,000/= (ambazo ofkozi ameshalipa, vinginevyo angeenda jela miaka mitatu). Pia kapigwa BAN la kuendesha gari kwa miaka mitatu. Ofkozi kuna "gharama" za uendeshaji wa kesi ambazo zilimgarimu kama 2m hivi, lakini maisha yanapaswa kuendelea.

Kwa ujumla, pokeeni salamu, shukrani na ahsante nyingi toka kwa mpiganaji Maskini_Jeuri.

Nawasilisha kwa upendo.

Mtumishi wenu mtiifu.

Asprin

Asante na pole zake nyingi! Ndo ukubwa huo mkuu
 
Pole MJ kwa yote yalikukuta pia tunashukuru Mungu yameisha salama.

Kumbe uchakachuaji upo mpaka kwenye srediii dah:doh::doh::doh:
 
Kwanii 'double road' ndio nini etii....?:confused2:
 
Pole MJ kwa yote yalikukuta pia tunashukuru Mungu yameisha salama.

Kumbe uchakachuaji upo mpaka kwenye srediii dah:doh::doh::doh:
MDOGO WANGU... KAMA HUJACHAKACHUA BADO POLE YAKO... JK alichakachuliwa mafuta pale moshi basi analipizia nchi nzima, kaanzia na kura, atarudi na mengine nyie subiri tu, tena nataka nimwalike awe memba wa jukwaa hili, tumkabidhi my dude Smiles
 
Haleluya Bwana apewe sifa. Tulizitanguliza pole nyingi kwa wafiwa hata MJ kwa yaliyowakuta. Kweli maisha hayana budi kuendelea zidi kuwa na matumaini. Lililosamehewa dunia hata mbinguni limesamehewa. Endelea kulisukuma gurudumu lako la maendeleo ni mapito katika maisha hatuna budi kukabiliana nayo.
 
MDOGO WANGU... KAMA HUJACHAKACHUA BADO POLE YAKO... JK alichakachuliwa mafuta pale moshi basi analipizia nchi nzima, kaanzia na kura, atarudi na mengine nyie subiri tu, tena nataka nimwalike awe memba wa jukwaa hili, tumkabidhi my dude Smiles

Wee! mnikabidhi mimi nani...??? sitaki....:mad2:
 
Yaani we acha tuu...
nimekumiss pia, ila huu uchaguzi umenikera hadi basi

yani kuna hii sura ya makame nikichanganya na sauti yake ndo nakereka zaidi,maskio yanasikia tu dovutwa!yamegoma majina ya wengine!
 
yani kuna hii sura ya makame nikichanganya na sauti yake ndo nakereka zaidi,maskio yanasikia tu dovutwa!yamegoma majina ya wengine!

Pole my dear.....ndio Tanzania yetu hiyo....
 
Back
Top Bottom