Salamu ni kitu cha muhimu sana hata kama hutaki kuongea na majirani zako

Think2

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2025
Posts
3,087
Reaction score
6,024
Hata kama uko busy sana jitahidi kusalimia majirani zako na sio kuwapita kama huwajui
Siku ukiugua ghafla na huwezi kushika simu kupigia ndugu ndio utajua umuhimu wa kuishi na majirani vizuri.
Note: Maisha ni yako sawa ila matanga ni yetu.
 
Malezi mabovu utampitaje jirani yako bila kumsalimia utakuwa lbd kichaa
 
Kama mtu ana utu atakusaidia tu bila masharti kama unasalimu watu au lah ila kwa watanzania hata ukiwa unawasalimia kila saa bado mioyo imebeba chuki likikufika ndo utajua hujui na hutoamini kiufupi tz tunaishi kiunafki sana.
 
Ni bora mgogoro wa wazi
 
mkuu mimi nilikuwa na mawazo kama yako,,lakini hapa nilipopanga kuna mmama mmoja akinikuta nipo nje hanisalimii,ameshawambia na dada zake na watoto wake kuwa wasinisalimie wala kunifungulia geti la kuingia kwenye nyuma,isitoshe huyu mama ana imani za kishirikina huwa analeta waganga hapa uwanjani katikati ya nyumba na wanatungua matunguli yao,,imefika hatua na mimi nimeona haina haja ya kumsalimia,,hivyo nataka nikwambie kuwa inategemeana na mtu
 
Malezi mabovu utampitaje jirani yako bila kumsalimia utakuwa lbd kichaa
Lakini yeye hazuiwi kukuhudumia ukipata shida. Atakua wa ajabu sana akiacha kukupa msaada kisa tu humsalimiagi. Ubinadamu ni kusaidiana, sio kusalimiana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…