Ki ukweli hata Mimi huwa sioni logic ya kutumia salamu nyingi kiasi hiki:
Asalaam Aleykum
Bwana Yesu asifiwe
Tumsifu Yesu Kristo
Mwanakondoo ameshinda
Nk nk nk
Ingetosha tu Kama ni Muislam asalimie kwa kadiri ya dini yake mara moja tu inatosha maana ukisema Asalaam Aleykum na mwingine akasema Bwana Yesu asifiwe lengo ni lile lile la kumtukuza Mungu kwa kadiri ya Imani yako, sio lazima useme salaam za dini zote.
Hiyo ya "Nawasalimu kwa jina la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania" nayo sioni Kama imekaa vizuri labda Kama iliwahi kupendekezwa na ilikuwa kwenye nyaraka zao huko ila binafsi naona sio salamu maana hata hatujui tunaitikiaje.
Binafsi naona salamu nzuri ni "Habari za saa hizi mabibi na mabwana" inatosha kabisa
Akipenda kama ni mchana,
Habari za mchana mabibi na mabwana
Asubuhi, habari za asubuhi mabibi na mabwana
Jioni, habari za jioni mabibi na mabwana
Hii ndo salamu inayotambulika hapa kwetu Tanzania ndiomaana hata wageni wanaotutembelea toka mataifa mengine tunawafundisha salamu hizo
Sijui kwanini viongozi wengi huwa wanapata kigugumizi kwenye salamu hii!
Wanapenda kujivika kilemba cha kusalimia kidini hata pasipohusika
Mungu yuko kila mahali na ni kweli kabisa lazima tumtangulize kwenye kila shughuli, lakini kwenye hii mikutano ya viongozi wa kiserikali itoshe tu kusalimia kwa salamu yetu ya kawaida
Kama Kuna viongozi wa dini watatufungulia shughuli yetu kwa sala inatosha kabisa
Alichokifanya Mama Samia jana ni kigugumizi tu cha asalimieje? Ukisoma body language, anaona kero kutamka salamu zote hizo wakati hata sio lazima. Kwa kadiri ya mazoea anaona akitamka moja na nyingine akaziacha atazua maswali mengi
Mimi naona haya hiyo ya Jina la muungano aachane nayo arudi kwenye salamu yetu ya siku zote "Habari za saa hizi" inatosha sana.