Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
Naibu Waziri wa Utamaduni sana na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma usiku wa Mei 16, 2023 nchini Afrika Kusini, amepata nafasi ya kufikisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wachezaji na benchi la ufundi la timu ya Yanga kuelekea kwenye mchezo wao wa mkondo wa pili wa nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika leo nchini Afrika kusini dhidi ya Marumo Gallants.
Akiongea na wachezaji pamoja na Benchi la Ufundi Mhe. Mwinjuma amewahakikishia kwamba Serikali ipo pamoja nao na amewataka kupambana ili kuhakikisha wanaingia fainali ya mashindano hayo.
Akiongea na wachezaji pamoja na Benchi la Ufundi Mhe. Mwinjuma amewahakikishia kwamba Serikali ipo pamoja nao na amewataka kupambana ili kuhakikisha wanaingia fainali ya mashindano hayo.