Poppy Hatonn
JF-Expert Member
- Apr 9, 2021
- 3,095
- 4,632
Ndugu wananchi,
Naona mwaka huu hamsheherekei Sikukuu ya Uhuru. Si kitu. Mradi tu mkumbuke kwamba mko huru.
Kwa sababu mimi na Rashidi na Oscar na Derek na Jamal na Maswanya na wengine wengi tuliwaletea Uhuru, tuliwaongoza katika harakati za kudai Uhuru
Kwa hiyo mjihadhari mtu yoyote asiwanyang'anye Uhuru wenu, kwa sababu uhuru ni zawadi ya binadamu kutoka kwa Mungu.
Mungu anataka kila mtu awe huru. Maendeleo ya nchi yanahitaji watu wawe huru.
Uhuru tuliowaletea ulikuwa ni Uhuru kutoka kwenye ukoloni, Watu Weupe walikuwa wanatutawala, kwa hiyo ilibidi tuwe huru, tuondokane na dhana kwamba Mtu Mweusi hawezi kujitawala, Mtu Mweusi anahitaji yaya.
Lakini viongozi mara nyingi hawapendi kabisa uhuru.
Wao wanatawala kwa mabavu na neno "uhuru" haliwafurahishi hata kidogo
Fikiria, kwa mfano, yule Rais aliyepita, mtu mjanja sana. Akaapishwa kuwa Rais, baada ya mwezi mmoja ikawa sherehe ya Uhuru, akasema sherehe ya Uhuru haitakuwepo, badala yake fedha za ile sherehe zitumike kukamilisha kipande cha barabara ya lami.
Watu wote wakaridhia, wakasema Rais anajali maendeleo ya nchi kuliko mambo ya anasa.
Halafu tazama baadaye alivyoiongoza nchi kwa Mkoko wa Chuma.
Ndiyo matatizo yanayotokea watu wanapouliza."Uhuru ni kitu gani, una faida gani kwangu?
Na Rais huyu wa sasa, anasema Uhuru usisheherekewe, badala yake anataka kuwajengea mabweni watoto walemavu. Okay, hatuna tatizo na hilo.
Lakini sasa ni wakati wa Uhuru, na kila mtu lazima ajiulize yuko huru kiasi gani.
Si kitu, si hoja kwamba hauko Segerea au Keko Ukonga. Kama haupo huru katika nyanja fulani, unakubaliana na maelezo unayopewa kwamba huna ruhusa kufanya hiki au kile, kwa sababu mambo mengine inawezekana kwamba unazuiwa kufanya kwa usalama wako mwenyewe.
Unakubaliana na mtu ambaye inaelekea kwako kwamba anakunyima uhuru, unakubali kwamba ana mamlaka, wadhifa wa kukunyima uhuru? Haya ni mambo ya kujiuliza, hasa wakati huu , ambapo nchi imepita katika kipindi cha udikteta;watu lazima wajiulize kama wako huru.
Kwa kawaida Sheria ya Nchi itaainisha kwamba yapo makosa makubwa ambayo raia hatakiwi kuyafanya.
Ikishaainisha makosa makubwa, baada ya hapo itaainisha makosa madogo ambayo mtu hatakiwi kufanya.
Hii Sheria ya Nchi ikishaainisha haya makosa madogo ambayo Rais hatakiwi kufanya, mtu hawezi kuibuka na kosa, akasema, hili pia ni kosa dogo ambalo hutakiwi kufanya.
Kwa sababu yale makosa madogo yameshaainishwa. Ingawa inatokea wakati mwingine kosa linatokea na bado halijatungiwa sheria, na hakimu inabidi atoe uamuzi kwa kadri anavyoweza, kwa sababu haruhusiwi kusema kesi imemshinda, au anayeshtaki na mshtakiwa wote wametoka sare.
Hivyo hivyo; mzazi, mlezi au kiongozi yoyote anapaswa kuainisha makosa makubwa na madogo, na asikurupuke kukataza kila jambo linalomkera.
Hivyo mtoto atajua amesimama wapi. Kama juzi Mkuu wa Wilaya amempiga kofi mtoto lakini anasema alimshika mkono tu.
Alimshika mkono tu wakati yule mtoto ana bendeji usoni? Lakini labda siyo vibaya kumpa nafasi huyo Mkuu wa Wilaya kuongea na huyo mtoto na mama yake.
Labda atafanikiwa kuwaeleza kwamba mtoto alishikwa mkono tu. Halafu labda tatizo linaweza kutanzuliwa bila media na sauti zao za tarumbeta.
Hii ni imaginary speech . Haijapokelewa kutoka kwa Mwalimu Nyerere verbatim ( neno kwa neno).
Nawasilisha. Sasa nasubiri vijembe