BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Akizungumza na Azam TV, Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC Salim Abdallah (Try Again) ametangaza kujiuzuru wadhifa wake.
Amewashukuru mashabiki na wajumbe wa bodi aliofanya nao kazi kwa ukaribu. Amewaomba wanachama wa Simba kuwa wamoja na kuondoa migogoro.
Aidha, amesema baada ya mashauriano mengi, yeye pamoja na wajumbe wenzake wameona Mo Dewji anafaa kuwa Mwenyekiti wa Bodi, na anatumaini atakubali ombi hilo.
Amesema anaondoka kwenye nafasi hiyo kwa bashaha, na yeye ni mdogo kuliko Simba. Pia, amemshukuru Mo kwa imani kubwa kwake na amewaomba wapenzi na mashabiki wa Simba kumpa ushirikiano wakati akianza kuisuka upya timu hiyo.
Try Again alianza kushika nafasi ya juu ya Uongozi ndani ya Simba SC 2017 kama Kaimu Rais wa Simba SC, Mjumbe wa Bodi na hatimae Mwenyekiti wa Bodi.
Pia soma:
- Tetesi: - Simba imepasuka. Kuna Simba ya Try Again na Simba ya Mo, Kila upande unauroga upande mwingine
- Tetesi: - Salim Abdallah ‘Try Again’ katika jaribio la kumng’oa Mo Dewj Simba!
- Tetesi: - Simba inatarajia kumrejesha tena Barbara Gonzalez kwenye Bodi
- Baada ya kumjua kuwa kumbe Adui Mkubwa wa Simba SC ni Mwekezaji Mo Dewji nawaomba Msamaha 'Mangungu' na 'Try Again'