View attachment 3014712
Akizungumza na Azam TV, Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC Salim Abdallah (Try Again) ametangaza kujiuzuru wadhifa wake.
Amewashukuru mashabiki na wajumbe wa bodi aliofanya nao kazi kwa ukaribu. Amewaomba wanachama wa Simba kuwa wamoja na kuondoa migogoro.
Aidha, amesema baada ya mashauriano mengi, yeye pamoja na wajumbe wenzake wameona Mo Dewji anafaa kuwa Mwenyekiti wa Bodi, na anatumaini atakubali ombi hilo.
Amesema anaondoka kwenye nafasi hiyo kwa bashaha, na yeye ni mdogo kuliko Simba.