Salim Kikeke: Ili ufikie Umahiri wa Kina Tido Mhando Lazima Ukwepe Kutumiwa

Yaani kisa kauliza maswali yanayokwaza chama chalk basi anakua low!!?..nyie wavaa kombati mna shida sana
Maswali gani yanakwaza chama? Ukijadili kwa ushabiki kama wa Simba na Yanga huwezi ona mapungufu ya uweledi katika kazi aliyofanya jana! Jana ameonyesha malengo yake kabisa yalikuwa nini, bahati mbaya kamkuta anaye muuliza ana uwezo 10x kumzidi ila ingekuwa wengine ni shida.
Kung'ang'ania eti Msigwa kasema mali za chama zinaibiwa yeye Lissu anasemaje, ni ujinga kuulizwa swali hilo toka mwandishi mbobevu anayejua fedha na mali za chama zinakaguliwa na CAG na ripoti inatolewa annually. Na anajua kuwa kila mwaka Chadema wanapata Clean certificate wakati vyama vingine vina hati chafu including CCM.
 
Na mimi nina maoni kama yako. Kasikilize mahojiano aliyofanya na Fatma Karume utamuonea huruma Kikeke. Niliona aibu mimi kwa sababu anaonekana kabisa anaogopa au amepewa misheni ya kuonyesha kuwatetea CCM/Samia. Akipewa jibu anakuwa kama anataka Fatma aongee anachotaka yeye.
 
Sikiliza mahajiano ya Fatma Karume na Kikeke. Huko siyo kuchokonoa bali ni ujinga na kujidhalilisha.
 
Shida ya watanzania mtu akihoji maswali chokonozi basi wa upande mwingine wanasema anatumiwa. Ingekuwa kamhoji maswali ya kichokonozi makamba hapo angepewa sifa na upande mwingine
Kila anayebisha namwambia asikilize mahojiano ya Kikeke na Fatma Karume. Wengine hata hamjui kinacholalamikiwa hapa. Kikeke yuko chini sana kimahojiano (pengine ni woga au anatumika).
 
Hapa bongo ukiwa serious sana unaweza jinyonga bro. So be simple kuwa na akili kidogo ujanja mwingi the rest will fight for themselves
 
Huyo Chawa tu...
Kumbukeni vyombo vya habari hapa nchini haviko huru kiasi hicho - mwandishi lazima aegemee upande wa watawala kidogo wakati anatengeneza maudhui ya mahojiano.

Ndiyo maana mahojiano haya yanamfurahisha mtu wa CCM na kumkera kiasi tu wa CDM.

Kwa mfano Mrema alisema.kabisa nakukuu "huenda Lissu kashaandika barua kwa katibu Mkuu ila mimi silifahamu hilo ma kama kashaamdika basi hajatengua kanuni yoyote ile ya katiba yetu:

Sasa Kikeke kangangania kwa nini katibu Mkuu hajamwambia msemaji? Hapa ndipo tatizo ka Kileke lilipo - si LAZIMA kwa Katibu mkuu kumwambia kila mfanyakazi wa ofisi yake kwamba kashapokea barua X za wagombea urais pamoja na majina yao.

Hoja hii alitaka kuikuza huyo Kikeke ionekane CDM wana gaps - wakati hamna hoja hapo.
 
anyway, nisibishe maana sijawahi msikiliza, ngoja nifanye homework hiyo
Mkuu @Retirwengi hapa wanajadili kitabu kwa rangi ya cover, ni kweli Kikeke alimhoji Lissu inavyotakiwa. Lakini anapofikia kumlisha maneno Mrema tofauti na alivyosema ni kama anajenga ugomvi ambao haupo! Na hilo kwa msikilizaji kama Kasuku hawezi lielewa.
Maswali ya zile kauli za Msigwa, majibu yako clear lakini anashikilia katika mfumo wa kuwa Msigwa ni mkweli hapo lazima tumtofautishe na mwandishi mtumia weledi.
 
Kupata clean certificate haimaanishi mali haziibwi,hapo inaonesha uchanga wako kwenye mambo serious,na jibu la swali la kikeke halikupaswa kuwa cag katoa clean certificate bali kujibu alivyodai msigwa kwamba mali zaibwa
 
Shida ya watanzania mtu akihoji maswali chokonozi basi wa upande mwingine wanasema anatumiwa. Ingekuwa kamhoji maswali ya kichokonozi makamba hapo angepewa sifa na upande mwingine
Anataka maswali ya kumfurahisha yeye tu, hawazi kua hayo maswali kuna wengine wanataka kusikia Lissu ana maoni gani..
 
Ni mbinu za interview. Unapigwa swali hili na lile kukuvuruga kuona umakini wako! Katika interview swali la msingi linazaa viswali vingi kama jibu halijitoshelezi. Sioni shida ya Kikeke hapo.πŸ™πŸ™πŸ™
 
Tido muhando huyo huyo amba ali bring creativity mka mfanya nini?
proble with you people mnaogopa competent individuals, manataka kutukuzwa kusifu kuabudu kama walivyo wengine
 
Umeiweka vizuri sana hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…