Salim Kikeke siyo kwa ubaya ila ni ushauri tu, punguza mbwembwe na mikogo

Salim Kikeke siyo kwa ubaya ila ni ushauri tu, punguza mbwembwe na mikogo

Huwa sipendi kufichaficha ujinga huu ulioandika pia ni ujinga kama ulivyoona wa salim kikeke nawe upo hivyo hivyo
 
Yaani ungeniambia Akina Yvonna Kamuntu ambaye taarifa ya habar toka inaanza mpaka inaisha ni kujitaja tuuuu mpaka unajiuliza ni anazuzuka na hii studio au , kidooogo ningalikuelewa but siyo KIKEKE SALIM hii ni mashine acha kabisaa
 
Mada ndefu Ila dhima kuu imejikita kwa Liverpool sio Kikeke
 
Kama kuna siku GENTAMYCINE umewahi kupost jambo lisilo na MASHIKO, nafikiri LEO ni KIBOKO. Au sio wewe WAJANJA WAMETUMIA JINA LAKO?
 
Kuna mtangazaji wa ITV kutokea Kagera anaitwa Audacy Mtabazi.


Hahahaha duniani kuna vituko sn
 
Ukisema Salim Kikeke ana mbwembwe, mtafute jamaa mmoja huwa anatangaza habari za biashara hapo hapo bbc anaitwa Aaron Heslehurst ndio utachoka. Mtafutr youtube ujionee mwenyewe.
 
Kila nilipokuwa nikimtizama hasa anatangaza Taarifa ya Habari ya Runinga ambayo huwa inarushwa na Kituo cha Runinga cha Star tv kila Jumatatu hadi Ijumaa Saa 3 Kamili hadi Saa 3 Unusu nilikuwa nikidhani labda huwa ni bahati mbaya tu lakini kadri ambavyo nazidi ' Kumkodolea ' nimegundua ya kwamba huyu Mtangazaji ameshalewa pongezi / kongole.

Ewe Mtangazaji wa BBC Swahili Salim Kikeke hizi mbwembwe zako zifuatazo huwa unamfanyia nani?

  1. Taarifa ya Habari ikianza tu unaingia kwa mikogo huku ukidundika
  2. Taarifa ya Habari ikianza tu kila mara unatuzungushia zungushia Kalamu kwa mikogo
  3. Taarifa ya Habari ikianza tu ukienda Kukaa unapiga Nne zisizo na maana hadi unaboa
  4. Taarifa ya Habari ikianza tu na ukiwa katikati mara unaanza kujiangalia ulivyovyaa
  5. Taarifa ya Habari ikianza tu kuna muda huwa unaingiza ' mizaha ' isiyo na maana / tija
  6. Taarifa ya Habari ikianza tu huwa unapenda kutaka kuwa ' dominate ' wenzio hadi katika taarifa zao na nadhani huwa ' wanakumaindi ' ila pengine wanakustahi au wanakuogopa
  7. Taarifa ya Habari ikianza tu kuna muda unaonekana ' Kukonyeza ' vimacho vyako sasa Sijui nani kakuambia kuwa wote wanaotizama hiyo News Bulletin yenu ni Wanawake tupu
Salim Kikeke ambaye nilikuwa nikimfahamu wakati akiwa Tanzania akitangaza katika Media aliyokuwepo na hata Salim Kikeke ambaye alikuwa akitangaza alipokuwa chini ya ' Manguli ' akina Mzee Tido Dustan Mhando na Charles Nkwanga Hillary kabla hawajamuachia ' mikoba ' siyo huyu wa leo.

Yaani Mzee Charles Hillary pamoja na ' Uhenga ' wake wote lakini akisoma taarifa ya Habari ya Azam tv anakuvutia na unamwelewa vyema huku ukiwa na hamu ya kuzidi kumtizama akitiririka na akiserereka Kiusomaji wa Habari na akiwa hana hata chembe ya ' Mbwembwe ' na ' Mikogo ' kama ambavyo Wewe ( Salim Kikeke ) unafanya.

Badilika ' Comrade '.

GENTAMYCINE ni kama Bahari ambayo siku zote huwa haikai na uchafu hivyo kama ' utanimaindi ' kwa haya niliyoyadokeza hapa ' Jamvini ' poa lakini najua nimekuwa mmoja wa ' Mashujaa ' wa kuwa tayari kukupa ukweli ambao najua na nina uhakika ukiufanyia Kazi huenda ukaja kuwa bora zaidi.

Na cha Kushangaza kama siyo Kusikitisha hata hao ' Wazungu ' wenyewe wenye hiyo BBC yao wakiwa wanatangaza taarifa zao za Habari huwa hawana ' mbwembwe ' na ' mikogo ' kama yako na bado huwa tunawaelewa sana tu sasa inakuwaje Wewe ' Wakuja ' tu huko ' Mamtoni ' uwe na ' mashauzi ' ya kupitiliza?

Halafu Weekend hii ukitutangazia mpira naomba unipe majibu kwanini huwa unaichukia sana Timu yangu pendwa ya Liverpool? Imekukosea nini? Kuna chochote labda unawadai wana Liverpool labda tujichangishe tukulipe ili uwe unaacha kutunanga / kutusema? Marefarii wa EPL watuchukie na Wewe tena utuchukie hivi Sisi wana Liverpool tutakuwa Wageni wa nani? Mbona huwa ' huzichambi ' Chelsea, Manchester United na Arsenal ambazo Kiuhalisia ndiyo Timu mbovu kuliko hata Liverpool?

Nawasilisha.
Inawezekana nyie ni watani wa jadi.
 
Back
Top Bottom