ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 25,030
- 61,298
Ukiwa na hela, ukiona watu wamejazana kwenye mahoteli wanakula bata unasema Uchumi unapiga hatua, watu wana pesa. Ukiwa huna hela unasema Hawa raia wanatoa wapi hela wakati hali ni mbaya hivi?
Ukiwa na hela, mafuta yakipanda bei unasema Hii ni hali ya soko la dunia Ukiwa huna hela unakuwa na makasiriko unasema Hii ni njama maalum ya serikali dhidi yetu.
Ukiwa na hela, kodi zikiongezeka unasema Hakuna maendeleo bila kodi. Ukiwa huna hela unasema Hii nchi imebaki kukusanya kodi tu.
Ukiwa na hela, ukiona jengo jipya la serikali unasema yes Maendeleo yanaonekana. Ukiwa huna hela unasema Hela zote zinaishia kwenye majengo.
Ukiwa na hela, umeme ukikatika dakika 10 unasema: "Mambo haya hutokea." Ukiwa huna hela ukisikia umeme umekatika mtaa hata ambako huishi unasema Nchi imeharibika kabisa.
Ukiwa na hela foleni unaiona sawa tu kwamba Mji umekua, shughuli za kiuchumi zimeongezeka. Ukiwa huna hela unaiona Hakuna anayejua anachofanya kwenye hii nchi.
Ukiwa na hela, ukiona viongozi wakisafiri nje unasema Wanatafuta wawekezaji.Ukiwa huna hela unasema Wanaenda kula hela zetu.
Ukiwa na hela, mshahara ukiingia unasema Tushukuru nchi ina amani.Ukiwa huna hela, sms ikikukumbusha deni lako unasema Tatizo la nchi hii ni mfumo mzima.
Ukiwa na hela unaamini kabisa kwamba maisha ni matokeo ya kufanya kazi kwa bidii. Ukikosa hela kwa miezi miwili unaanza kusoma thread za jukwaa la intelligence siri za Illuminati na mfumo kandamizi wa dunia
Ukiwa na hela, ukiona mtu amefanikiwa unasema Hongera zake, amejituma.Ukiwa huna hela unasema Hapo lazima kuna mkono wa mtu.