Sallam akanusha WCB kuwa na ugomvi na Clouds Media

Sallam akanusha WCB kuwa na ugomvi na Clouds Media

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Dar es Salaam. Mmoja wa mameneja wa Nassib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, Sallam Sharaf amekanusha kuwa na matatizo na uongozi wa Clouds Media Group na kwamba wana ushirikiano mzuri wa kikazi.

Minong’ono ya kuwepo kwa tofauti kati yao ilianza mapema leo Februari 7, 2018 baada ya mfululizo wa posti katika mtandao wa kijamii wa Instagram unaohusisha pande zote mbili, wakihusisha tukio la madai ya kushambuliwa kwa watangazaji wa kipindi cha Shilawadu kinachorushwa na televisheni ya Clouds.

Sallam aliandika waraka aliouambatanisha na picha ya Diamond akisema: “Kumbe tatizo ni kumpoteza huyu kijana? Waambie familia yako na wazazi waliokuleta katika haya maisha huyu mtoto kaletwa kwa makusudi maisha haya, ili kuleta ukombozi wa dhuluma uliyokuwa unaleta kwenye Taifa hili, unatikiwa kujua Kwanza hili Taifa sasa Rais anaitwa John Pombe Magufuli.”

Saa sita baadaye dansa wa Diamond, Mose Iyobo aliposti picha akiwa na Diamond na kuandika: Nishapoa simba ila lengo lao ni wewe mie kioo tu.”

Kauli hizo zimewavuta mashabiki mitandaoni waliohusisha kauli hizo na sintofahamu iliyoibuka wiki iliyopita hasa baada ya watangazaji wa Shilawadu kudai kuwa wameshambuliwa na Iyobo, madai ambayo dansa huyo ameyakanusha.

Sallam amesema yanayoendelea ni mambo ya kawaida na hakuna bifu ndiyo maana Clouds televisheni na redio wanacheza nyimbo za wasanii wa WCB kama kawaida, ameahidi kutoa taarifa rasmi baadaye leo.

“Msiwe na haraka, tutatoa statement (taarifa) muda si mrefu na tutawatumia wote, ”amesema Sallam.

Chanzo: Mwananchi
 
ruge mbona anawaendesha sana ? wasanii wa bongo hawaamini kwamba hawawezi kutoka bila ruge ? ana nn huyo watu wanamtetemekea ?
wcb tayari ni brand kubwa, walipofika kwa sasa ruge hawezi kuwafanya lolote , wajielewe hawa watu.
 
Threads za watoto wa Kinondoni hizi.

Nitarudi baadae kuja kusoma replies.
 
Ukikosana na clouds believe me huwez ku survive kamwe na mifano ipo mingi we fikilia kuna EATV,EFM,MAGIC FM,RADIO ONE, R.F.A na nyingine kibao tu nyingine kubwa nikoani ukikosana na clouds wote hao wanapiga nyimbo zako.Lakini nyimbo yako isipopigwa CLOUDS ndo mwisho wako jiulize kwa nini
 
Hizo zama zimeshaisha,huu ni wakat wa social media,watu wanafata nyimbo mitandaoni hata usipopiga watazipata tu.
 
Hizo zama zimeshaisha,huu ni wakat wa social media,watu wanafata nyimbo mitandaoni hata usipopiga watazipata tu.
Nenda simiyu mkoa mpya uone Kama kuna radio moja tu nayo ni clouds ndo inasikika mwanzo mwisho
 
Ukikosana na clouds believe me huwez ku survive kamwe na mifano ipo mingi we fikilia kuna EATV,EFM,MAGIC FM,RADIO ONE, R.F.A na nyingine kibao tu nyingine kubwa nikoani ukikosana na clouds wote hao wanapiga nyimbo zako.Lakini nyimbo yako isipopigwa CLOUDS ndo mwisho wako jiulize kwa nini
Naona umejikatia tamaa kabisa mkuu....
 
Ukikosana na clouds believe me huwez ku survive kamwe na mifano ipo mingi we fikilia kuna EATV,EFM,MAGIC FM,RADIO ONE, R.F.A na nyingine kibao tu nyingine kubwa nikoani ukikosana na clouds wote hao wanapiga nyimbo zako.Lakini nyimbo yako isipopigwa CLOUDS ndo mwisho wako jiulize kwa nini
Naona umejikabidhi mazima kwa mwanamume mwenzio.
 
Back
Top Bottom