Sallam athibitisha Harmonize kujiondoa WCB

Atakamata soko la Lindi, Mtwara, Masasi mpaka Nachingwea yote. Nangumene wote lazima wampe support wa nyumbani.
bila kusahau nanjilinji, nakapanya, miguruwe n.k
 
kweli mzee..wcb ndo ilikua kila kitu kwake sasa amenyea kambi atakua kama mavoko

halafu mbaya media zingine pia haziivi sa cjui nae atafungu radio na tv
Time will tell atarudi kuwalaumu Wasafi ndio wanamkwamisha.. Hamo hana talent ya kusimama nje ya Wasafi evidence project yake na Q chilla imeangukia pua pamoja na mkwanja mrefu alioweka
 

M Sizan km iko hivyo kwa sababu mkurugenzi mkuu wa kampun ni yeye diamond ana mameneja wa tatu na kl msanii anameneja wake kwaiyo wcb cio ya fela au salamu wote wanategemea mshahara kutoka kwa mond Ndiyo ambae wana mmeneji
 
Duuh kama ndio hivi bora ajitoe kwnye iyo ndoa haramu
mikataba ya kichifu kimangungo. nilishawahi kuratibu event moja ambayo tulimualika mbosso kuja ku perform. dogo alijituma sana stejini mpaka akakaukiwa sauti.

nilihuzunika sana niliposikia licha ya kujituma kwake kote kule, asilimia karibia 70% ya pesa tuliyomlipa ilienda kwa hao jamaa watatu na management ya wasafi.
 
M Sizan km iko hivyo kwa sababu mkurugenzi mkuu wa kampun ni yeye diamond ana mameneja wa tatu na kl msanii anameneja wake kwaiyo wcb cio ya fela au salamu wote wanategemea mshahara kutoka kwa mond Ndiyo ambae wana mmeneji
Kuna interview Fela alishasemaga kila show wanayopiga wanagawana hao wote
 
kweli mzee..wcb ndo ilikua kila kitu kwake sasa amenyea kambi atakua kama mavoko

halafu mbaya media zingine pia haziivi sa cjui nae atafungu radio na tv
Acheni ramli wakuu

Dogo amekuwa mkubwa sasa
Acha ajisimamie kazi zake

Wewe mwenyewe huwezi kula kwa baba na mama miaka yote; kuna umri ukifikia chakula chao utakionea aibu.

Wacheni akatafute changamoto mpya.
 
jembe ni jembe hawezi kuangushwa na hao wavuta bangi kamwe
 
Na awashukuru sana WCB kwa kuwekeza pesa nyingi kwake vinginevyo yangekuwa yaleyale ya BSS.
Very true, sasa ile machinery iliyokuwa ikiusukuma muziki wake ndiyo ataikosa.
Kama ameanza kwa kukwama vitu vidogo kama USA visa, ajipange sana.
Najua kuna Godfather somewhere aliyemuahidi kuwa nguzo on mutual benefits kibiashara lakini game ya muziki ina mambo mengi, all in all tumuombee asirudi kwenye 'kuvaa kandambili' kule alipotokea.
 
No situation is parmanent. Namuona Harmonise akienda kuwa mwanamziki mwenye mafanikio na historia kubwa.

Ana jiamini, ni jasiri, ana utayari.

Kamwe huwezi kuyafikia mafanikio makubwa ya leo kama hutakuwa na hutafanya tofauti na jana.
pia jamaaa ni mbunifu sana
 
Mafahali wawili hawakai zizi moja! Hamo na Mond wote wakubwa
Eti Hamo mkubwa,since when? Hata Mavoko ilisemwa hivyo hivyo kwamba kajishusha kaenda WCB wanamfanyia fitna asimpite Diamond kiwango sasa sijui nini kimemsibu manake afadhali alivyokuwa WCB alionekana kuanza kung'ara lakini sasa kapotea jumla.
 
Msanii wa kundi la WCB Harmonize ameandika barua ya kujiondoa kundi la wasafi kulingana na maelezo ya afisa mtendaji wa wafasi Sallam SK.

Akizungumza kupitia wafasi tv/wafasi fm Sallam SK amesema kuwa Harmonize ameandika barua ya kujiondoa kwenye kundi hilo japokuwa bado ana mkataba na kundi hilo.

Msanii Harmonize amesema kuwa yupo tayari kupitia vifungu vyote vya mkataba wake na wcb ili ajiondoe kwenye kundi hilo.

Kulingana na maelezo ya Sallam SK ni kuwa msanii Harmonize moyo wake haupo tena WCB na hata vitendo vyake haviendani na ule ushirikiano uliopo wcb, Sallam SK amemuomba msanii harmonize kuondoka salama wcb bila kuanzisha vurugu kwenye kundi hilo.

Source: bbc swahili
source: mwananchi
 
Ruge na Kusaga si ndio walewale!? Acha kuchekesha.
 
At least wewe umeandika kitu chenye sense, kuenda tena kuwa chini ya mtu sidhani kama ni move nzuri.
Angeazisha lebel ikikomaa ndiyo aage jumla jumla, kwa sababu angekuwa anaiangalia inavyokwenda(trend) huko akiwa na strong pillar(lebel aliyosainiwa WCB) kuhakikisha mambo yake yanaenda bila mikwaruzo.
Ila guts za kujilipua huwa ni nzuri sometimes, hapo hatujajua Sebastian amemuahidi nini au terms zao za makubaliano zikoje. Goodness Sebastian anamchukua dogo wakati tayari ana jina kubwa hivyo mkataba wao utakuwa balanced kwenye percentages watakazokubaliana.
 
Af watu hamjui uzito wa LEBEL mfano KANYE WEST na mipesa yake yote ile lakini yupo chini ya Jay Z na halalamiki na anakatwa asilimia flani kama kawaida.

ukiona mtu halalamiki kwenye record lebel ujue terms and conditions katika makubaliano yao inatao favour kwa kila upande.

hii ni tofauti na aina ya mikataba yenu mnayoingia na wasanii huku bongo. mnawabana sana hawa vijana kwenye mikataba. mnalifanya hili kwa kuwa wengi wao hawajaenda shule.

na kwakuwa wengi wao ni zero brain academically, wanakuwa too excited na ile lifestyle ya kuishi kisuper star(kuvaa nguo nzuri, kuendesha gari, kudate na wadada maarufu wa mujini nk). huwa hawatilii maanani vipengele vya kwenye mkataba. wanakimbilia kusign kichwakichwa.

baada ya miaka kwenda mbele, baadae wanakuja kushtuka kuwa wanadhurumiwa, hawafaidiki na kazi zao. wanashtuka kuwa wanamtajirisha mtu au kikundi fulani cha watu wachache. inawezekana hiki ndio kilichomsukuma harmonize kuvunja mkataba na wasafi.
 
Ni wakati wa Konde boy kula kwa jasho lake,

Kila jema limtangulie In Shaa Allah/
Anatakiwa kupigana sana hakuna mtelezo tena,

Kutofanya vizuri kwa project yake na Chilla aichukue kama tahadhal ya kilichopo mbele yake.
Hata ile aliyofanya na Country boy naona imefeli pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…