Sallam athibitisha Harmonize kujiondoa WCB

Ruge na Kusaga si ndio walewale!? Acha kuchekesha.
ktk michongo ya kimafia, inafika kipindi mafia kwa mafia huwa wanazidiana mbinu.

ni kweli hakuna aliye nafuu kati yao ila nilichotaka kusema ni kwamba sallam, tale na fella kiboko yao katika mbinu na makakati alikuwa ruge. ruge alikuwa na mbinu nyingi za kumu win out mshindani wake wa kibiashara.

kiufupi ni kwamba ruge mmoja ni sawasawa na ukusanye akina sallam kumi. mpaka sasa bado hajapatikana mbadala wake.
 
jembe ni jembe hawezi kuangushwa na hao wavuta bangi kamwe
jembe ni jembe alikua zamani, Nenda mwanza kaulize, Kila Kona ilikua jembe. Kwanini jembeka festival haipo? Huenda jembe anamtegemea harmonize ku boost biashara zake.

Tumpe muda Ila namuombea Kila la kheri harmonize ili tuwe na wasanii wakubwa wengi.
 
Bora sisi team kiba.. wazee wa kings music [emoji445] mambo yetu sio mengi kabisa..
#Rhumba
 
Mwisho wa siku inabidi mtambue kuwa WCB sio kundi bali ni music label! Kila mtu ana uhuru wa kuwa na management yake! Kama ameamua kuodoka ina maana kaona label yake haiwez kumfikisha kule anapotaka kufika. Huenda anaanzisha label yake mwenyewe tofauti na WCB itakayomfikisha mbali yeye na kuwainua wasanii wengine.

Mbona Diamond alipoachana na management yake ya mwanzo na akaanzisha label yake na managers wake kuna watu walisema anapotea ila matokeo yake amepiga hatua kubwa sana na akawatoa wasanii wenzanke hadi level za kimataifa kama akina Harmonize, Rayvany na wengine?

Kwa nini yeye Harmonize asifungue ya kwake na akawachukua wasanii wengine na kuwa push kufikisha mziki wao nje ya Africa kama alivyofanya Diamond? Hii ndio maana halisi ya kuthamini kudaidiwa (na wewe kusaidia wengine)

Hivi nyie mnafurahi kuona mziki wetu unabebwa na hawa wasanii wawili watatu tu nje ya Tanzania? Hamna kiu ya kuona akina Diamond wengine??

Na kama mna kiu ya kuona akina Diamond wengine mnategemea ni msanii mwingine anaweza kuwa na nguvu kama Diamond kama sio Harmonize? Alikiba ambae ndo tulimuona kama msanii mkubwa wa kuwapeleka wengine nje ya Africa amedevela, hata yeye kashindwa kujifikisha huko!

Lakini pia Diamond anahitaji mshindani haswa! Na WCB wanahitaji label nyingine itakayotoa ushindani mkali! Ushindani huu utapeleka mziki wetu mbali zaidi na zaidi.

BTW wenzetu wamechoka kusikia neno WCB katika kila nyimbo inayobamba nje! Huko nje tunaonekana hatuna studios za maana zaidi ya zile za WCB, hatuna wasanii wa maana zaidi ya wale wa WCB!
Wenzetu Nigeria ukisikia au kuangalia nyimbo zao studios zao nitofaut tofauti, video directors wao ni tofauti tofauti na labels ziko nyingi!

Kila la heri kwa Kondeboy. Sisi mashabiki wa WCB tutaendelea kukupa support ya kutosha maana tunautakia mema mziki wetu. Achana na hao wanaothamini kulamba miguu ya mtu bila kuangalia mbele.
 
Namtakia kila la kheri Harmonize!
Kama ameona WCB hawawezi mfikisha anapo pahitaji basi si vibaya kwenda kuangalia njia nyingine!
Well said Mkuu, ila ukweli wa wazi ni kwamba hapa Bongo sijaona lebo nyingine zenye nguvu ukilinganisha na WCB katika kusimamia wasanii, na hili ni tatizo linadidimiza ukuaji wa sanaa ya muziki wa bongo fleva.

Tuna hitaji lebo nyingi zenye nguvu na ushindani. Mfano Harmonize anatoka WCB anaenda lebo ipi?
 
Acha usaniii..hizo nyimbo huwa zinachezwa station gani, au club gani sisi tusizisikie. Huyo lavalava amefail sana. Unabebwa na lebo kubwa bado unashindikana!!!! Bora wasafi wangetupa hii takataka wakakaa na Marioo.
 
Acha usaniii..hizo nyimbo huwa zinachezwa station gani, au club gani sisi tusizisikie. Huyo lavalava amefail sana. Unabebwa na lebo kubwa bado unashindikana!!!! Bora wasafi wangetupa hii takataka wakakaa na Marioo.
Marioo hawezi kukubaliana na mikataba ya ajabu ajabu labda dudubaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…