Hatimaye Meneja wa Wasfi Classic Baby (WCB), Sallam SK amekata mzizi wa fitna baada kuthibitisha Harmonize kaandika barua ya kuvunja mkataba na lebo ya WCB.
Amesema kwa sasa wanasubiria kufanya taratibu za kisheria kuuvunja mkataba na karibuni watakuwa na kikao cha kukubaliana 'terms' ingawa Harmonize ameshaonyesha nia ya kukubaliana na 'terms' zote za kuvunja mkataba.
Sallam ameomba radhi kwa mwenendo uliokuwa unaonyeshwa na msanii huyo siku za karibuni lakini amewaomba mashabiki wa Wasafi waendelee kutoa ushirikiano kwa Harmonize kwani ajaondoka kwa ubaya.
Sallam amesema katika tamasha la Wasafi lililofanyika mjini Mwanza, Harmonize alitumia usafiri binafsi, kufanya baadhi ya mambo yaliyotoa tafsiri kuwa amejitenga.
Sallam amesema kwa sasa Harmonize moyo wake haupo Wasafi lakini ukweli ni kuwa bado ana mkataba na kundi hilo.
Kuhusu kujitenga na wenzake Sallam amesema, “Hili jambo si sawa kulingana na maudhui ya tamasha hilo. Maudhui ya Wasafi Festival ni umoja. Msanii akiamua kuacha kuambatana na wasanii wenzake ambao wapo pamoja katika tamasha ni kwenda kinyume.”
“Sisi katika tamasha letu hatupendi kutengeneza matabaka, tumeamua kuwa kitu kimoja, siyo kwamba Diamond, Rayvany hawakuwa na uwezo wa kutumia usafiri wao binafsi kama alivyofanya Harmonize” amesema Sallam.
Mtazamo wangu;
Harmonize anaenda kuwa historia kwenye muziki wa bongofleva uenda tukashangaa sana pale ambapo hatutasikia tena muziki wa kueleweka kutoka kwake na ukawa mwisho wake kisanaa.
Waliomshauri Hamo anapaswa kuwachukia maisha yake yote kama waliomshauri Mavoko.
Mwisho wa siku inabidi mtambue kuwa WCB sio kundi bali ni music label! Kila mtu ana uhuru wa kuwa na management yake! Kama ameamua kuodoka ina maana kaona label yake haiwez kumfikisha kule anapotaka kufika. Huenda anaanzisha label yake mwenyewe tofauti na WCB itakayomfikisha mbali yeye na kuwainua wasanii wengine.
Mbona Diamond alipoachana na management yake ya mwanzo na akaanzisha label yake na managers wake kuna watu walisema anapotea ila matokeo yake amepiga hatua kubwa sana na akawatoa wasanii wenzanke hadi level za kimataifa kama akina Harmonize, Rayvany na wengine?
Kwa nini yeye Harmonize asifungue ya kwake na akawachukua wasanii wengine na kuwa push kufikisha mziki wao nje ya Africa kama alivyofanya Diamond? Hii ndio maana halisi ya kuthamini kudaidiwa (na wewe kusaidia wengine)
Hivi nyie mnafurahi kuona mziki wetu unabebwa na hawa wasanii wawili watatu tu nje ya Tanzania? Hamna kiu ya kuona akina Diamond wengine??
Na kama mna kiu ya kuona akina Diamond wengine mnategemea ni msanii mwingine anaweza kuwa na nguvu kama Diamond kama sio Harmonize? Alikiba ambae ndo tulimuona kama msanii mkubwa wa kuwapeleka wengine nje ya Africa amedevela, hata yeye kashindwa kujifikisha huko!
Lakini pia Diamond anahitaji mshindani haswa! Na WCB wanahitaji label nyingine itakayotoa ushindani mkali! Ushindani huu utapeleka mziki wetu mbali zaidi na zaidi.
BTW wenzetu wamechoka kusikia neno WCB katika kila nyimbo inayobamba nje! Huko nje tunaonekana hatuna studios za maana zaidi ya zile za WCB, hatuna wasanii wa maana zaidi ya wale wa WCB!
Wenzetu Nigeria ukisikia au kuangalia nyimbo zao studios zao nitofaut tofauti, video directors wao ni tofauti tofauti na labels ziko nyingi!
Kila la heri kwa Kondeboy. Sisi mashabiki wa WCB tutaendelea kukupa support ya kutosha maana tunautakia mema mziki wetu. Achana na hao wanaothamini kulamba miguu ya mtu bila kuangalia mbele.