Sallam athibitisha Harmonize kujiondoa WCB

Sallam athibitisha Harmonize kujiondoa WCB

Swadakta; kwa asiejua watu wa huku kusini atasema unalopoka ila mm pia mmakonde natoa ushuhuda ni kweli watu wa huku wana ushikaji fake km hawana wanajishusha utawaonea huruma ila siku akifanikiwa nakuambia huruma yako itakuponza si tuna ujanja wa kukulupuka na kujiona zaidi kwa Tanzania hii naamini sisi ndo mabingwa wa kulipa wema kwa ubaya
Harmonize amesitisha ushkaji na WCB au amesitisha mkataba na WCB??

Tuanzie hapa kwanza.
 
Hatimaye Meneja wa Wasfi Classic Baby (WCB), Sallam SK amekata mzizi wa fitna baada kuthibitisha Harmonize kaandika barua ya kuvunja mkataba na lebo ya WCB.

Amesema kwa sasa wanasubiria kufanya taratibu za kisheria kuuvunja mkataba na karibuni watakuwa na kikao cha kukubaliana 'terms' ingawa Harmonize ameshaonyesha nia ya kukubaliana na 'terms' zote za kuvunja mkataba.

Sallam ameomba radhi kwa mwenendo uliokuwa unaonyeshwa na msanii huyo siku za karibuni lakini amewaomba mashabiki wa Wasafi waendelee kutoa ushirikiano kwa Harmonize kwani ajaondoka kwa ubaya.

Sallam amesema katika tamasha la Wasafi lililofanyika mjini Mwanza, Harmonize alitumia usafiri binafsi, kufanya baadhi ya mambo yaliyotoa tafsiri kuwa amejitenga.

Sallam amesema kwa sasa Harmonize moyo wake haupo Wasafi lakini ukweli ni kuwa bado ana mkataba na kundi hilo.

Kuhusu kujitenga na wenzake Sallam amesema, “Hili jambo si sawa kulingana na maudhui ya tamasha hilo. Maudhui ya Wasafi Festival ni umoja. Msanii akiamua kuacha kuambatana na wasanii wenzake ambao wapo pamoja katika tamasha ni kwenda kinyume.”

“Sisi katika tamasha letu hatupendi kutengeneza matabaka, tumeamua kuwa kitu kimoja, siyo kwamba Diamond, Rayvany hawakuwa na uwezo wa kutumia usafiri wao binafsi kama alivyofanya Harmonize” amesema Sallam.


Mtazamo wangu;

Harmonize anaenda kuwa historia kwenye muziki wa bongofleva uenda tukashangaa sana pale ambapo hatutasikia tena muziki wa kueleweka kutoka kwake na ukawa mwisho wake kisanaa.

Waliomshauri Hamo anapaswa kuwachukia maisha yake yote kama waliomshauri Mavoko.
Mitizamo ya namna hii inaweza ikawa sawa ama sio sawa! na hawa ni baadhi ya wale watu wanaopata taabu wakiwa makazini lakini wanasema nitakwenda wapi bora nikomae hapa hapa mwisho wasiku wanapelekwa mirembe au wanajikuta wamejinyonga vichakani kwa kuvumilia stress! Jitume sema naweza pambana mwenyewe bila fulani maisha yataenda vile ulivyokadiriwa na juhudi zako pia! Wake up !!
 
Hujanielewa Mkuu, nimemanisha kwa Sallam msanii wa kwanza kumsimamia kazi zake (hata kama ni baadhi) alikua AY, na alimfikisha level za International
Kwa wimbo upi unamaanisha mkuu alimfikisha international na ni lini?
 
Itafute speak with your body
Kwa wimbo upi unamaanisha mkuu alimfikisha international na ni lini?
Sujawahi ona collable kali kama ile kibongobongo,,unaweza kusema nibdude la usa hivi kumbe ni ambwene
 
Itafute speak with your bodySujawahi ona collable kali kama ile kibongobongo,,unaweza kusema nibdude la usa hivi kumbe ni ambwene
Si kweli unaizungumziaje African beauty ya Diamond au ule Diamond ameshirikisha Neyo na huo sio wimbo wa kwanza wa AY international
 
Kwa wimbo upi unamaanisha mkuu alimfikisha international na ni lini?
Inaonekana sio mfatiliaji wa mambo ya bongo flavor, ok kukusaidia kuna Uzi humu utafute Sallam alifanya interview na Champion utaelewa nachokwambia
 
Inaonekana sio mfatiliaji wa mambo ya bongo flavor, ok kukusaidia kuna Uzi humu utafute Sallam alifanya interview na Champion utaelewa nachokwambia
Mbona ni logic ndogo mkuu kama unajua unajibu na mim nikupe facts ninazozifahamu hata Diamond anajua ni nani alimconnect level ya kiafrica hadi international wala hawezi kukuambia ni Sallam huyo anatumwa tu nenda pale kafanye hiki watu tayari washaset mambo
 
Hahaha Tuwekeane screen shot za Bank Balance Mimi na wewe ..



You're Such a certified Poor .. You'll Frankly Die Poor .. We piga domo hela nimeyolaza leo utaipata after 4 months kama unafanya kazi ila kama unaishi na kulala kwenye masofa ya shemeji yako endelea kumsihi Dada yake aongeze speed ya kiuno upate kufugwa kama Kuku la kichina.



Utakufa fukara mbwa wewe.View attachment 1187941
Matajiri au wenye hela huwa hawafanyi upumbavu kama huo sana sana utawaona kwenye ku spend pesa zao sio kuonyesha figures za kupakua mtandaoni kama unavyofanya mpuuzi wewe

You are a certified mpumbavu.
 
Na sababu hasa ni hiyo! Badala ya kutaka watu wavunje miiko na kushindana na wanigeria mnataka muendelee kubweteka huku mkijisemea kauli zenu hizo za kizembe na kujinung'unisha eti "wanigera wametuzidi mbali sana"

Dawa ni kuthubutu na sio kulamba miguu ya watu.

Mbona Diamond mwenyewe alitolewa na Davido kimataifa lakini sasa hivi hawaelewani vizuri kama mwanzo? Unafikiri ni kwa nini?

Chagua moja uendelee kuelewana na aliyekutoa ukimlamba miguu ubaki hapo hapo au mtofautiane ili upige hatua zaidi.

Nadhani umenielewa vizuri sana
Unaweza kuthibitisha kwamba Diamond na Davido hawaeleweni au umeokota maeneo ya mtaani ya kuyaleta hapa kama yalivyo.
 
Mitizamo ya namna hii inaweza ikawa sawa ama sio sawa! na hawa ni baadhi ya wale watu wanaopata taabu wakiwa makazini lakini wanasema nitakwenda wapi bora nikomae hapa hapa mwisho wasiku wanapelekwa mirembe au wanajikuta wamejinyonga vichakani kwa kuvumilia stress! Jitume sema naweza pambana mwenyewe bila fulani maisha yataenda vile ulivyokadiriwa na juhudi zako pia! Wake up !!
Hii comment nahisi kama imeandikwa kunilenga mimi mkuu. Kuna mambo umeandika hapo inabidi niyafanyie kazi.
 
Me napenda tu kumtakia kila la kheri Harmonize, kwa safari yake nyingine anayotaka kuianzisha katika mziki wake......nje ya WCB.

And Infact naona hajafanya vibaya kutaka kutoka pale WCB...so tuendelee tu kusupport kazi zake.
 
Fact.
Harmonize ni lini aliuza mitumba Tandale? Hii ni fact ndogo ambayo inaondoa maana ya yote uliyoyaandika.

Nawashangaa sana mnaosema Harmonize kakosea kubadili management... Hivi nyie mnaijua WCB kuliko Harmonize?
Harmonize ni mtu wa ndani wa WCB, anajua mengi kuliko mtu yeyote nje ya WCB. Acheni kuleta siasa ktk masuala ya career za watu.
Huu uchambuzi wenu hauna maana yoyote maana tasnia ya muziki inahusisha mambo ya ndani ambayo hatuyajui tofauti na mpira unaochezwa hadharani ndio maana mtu unaweza kufanya uchambuzi ila sio muziki wetu uliobeba fitna za kila namna.

Mimi naona tumtakie heri kijana wetu, ameonesha uthubutu muacheni asonge mbele acheni hizi ramli zenu chonganishi.
 
Back
Top Bottom