Salma Kikwete ataka Sheria ya Stahiki za wake wa Viongozi Wakuu

THE FIRST BORN

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2019
Posts
2,224
Reaction score
4,472
Habari!
Hii taarifa imenipata nikaona niilete kama ilivyo.

My Take: Yani wanataka kila kitu serikali iwaandalie yani hadi Future yao kweli?

Mbunge wa Mchinga (CCM), Salma Kikwete ameishauri Serikali kutengeneza utaratibu ama sheria ya kuwahakikishia stahiki zao wake na wenza wa viongozi wa juu, akiwemo Rais, mara baada ya wenzi wao kuchaguliwa kushika nafasi hizo.

Mbunge huyo ambaye ni mke wa Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete ameyasema hayo leo Ijumaa Aprili 22,2022 Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia katika makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mwaka 2022/2023.

Amesema wake wa viongozi akiwemo rais, makamu wa rais na Waziri Mkuu mara baada ya wenza wao kushika nafasi hizo wanatakiwa kustaafu na kuendelea na shughuli nyingine.

Amesema kitendo hicho kinamaanisha kuwa utaalamu wake unatoweka.

“Ukiwiwa sana unaweza kusema hebu nianzishe Ngo (mashirika yasiyo ya kiserikali) lakini hata ukianzisha hakuna mtu anayeku suport ni wewe mwenyewe uhangaike ili kuhakikisha unapata raslimali ili uweze kuendesha Ngo,”amesema.

Ameomba Serikali kutengeneza utaratibu wa kisheria ambao mke wa kiongozi anapomaliza muda wake ajue ni nini anachotakiwa kukifanya.

“Ni imani yangu mtatengeneza utaratibu ama sheria inayomuhusu mke wa Rais ama wenza nini bada ya hapo kiendelee kufanyika ni jambo muhimu sana na si kwangu bali ni kwa vizazi vijavyo kujua haki zao,”amesema.

Chanzo: MWANANCHI
 
Kwani hicho atakachokua ameandaliwa mume au mke 'samia' hakikupangwa kula na familia yake. Watuondolee ulaku wao. Wamelamba asali hadi hawataki tena uwepo utawala wa kutetea umma na wanyonge kwenye jamii.
 
CCM oyee! Mkiambiwa CCM ni majizi yanayoangalia matumbo yao huwa hamuelewi. Wanyongee endeleeni kuvalishwa khanga na kuchezeshwa michiriku wakati wa kampeni hayo ndio matokeo yake.

Badala ya kuangalia future ya taifa na ya kizazi hiki na vijavyo ukiwa ndani ya chumba cha kupigia kurua; endelea kukumbuka ulanzi, dengerua, mnazi, bia, ubwabwa sijui pilau ulilolishwa jana kwenye kampeni! Ujinga ni tatizo kuu la nchi hii! Unajiuliza mtu kama huyu alipenyapenyaje hadi kuingia mjengoni; ni sababu ya jina? Ana akili sana? Ujinga wa wapiga kura? Rushwa? Au?
 
Genge la mizoga ya msoga linazidi kutafuna tu!

Huyu nae anataka kiinua mgongo?

Hajaridhika tu jinsi basha wake alivyopora mapesa ya nchi kwa miaka kumi?

Na bado ubunge tukampa, na mwanae muuza madawa nae tukamtunuku ubunge wa bure!

Hashibi tu!?
Itafikia hatua wataomba hadi wajukuu zao waandaliwe mazingira mazuri Babu zao wanapostaafu Urais
 
Mkuu hii nchi ina viongozi wa ajabu sana hawaoni hata hali ya saiv ilivyo ngumu wanawaza kutengenezewa sheria za wao kuendelea kunufaika.
 
Hicho kitu hakiwezekani, tunaweza pata rais akamuoa dada yake ili apate stahiki au rais akamroga mke mkubwa ili nyumba ndogo arithi stahiki, au nyumba ndogo ikamroga mke wa rais ili aolewe apate stahiki. Ni kama ilivyo kwa makamu wa rais kwa sasa ktk katiba, ni rahisi sana makamu wa rais kumuua rais ili awe rais kwa sababu katiba inaruhusu makamu wa rais kuwa rais moja kwa moja badala ya uchaguzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…