Habari!
Hii taarifa imenipata nikaona niilete kama ilivyo.
My Take: Yani wanataka kila kitu serikali iwaandalie yani hadi Future yao kweli?
Mbunge wa Mchinga (CCM), Salma Kikwete ameishauri Serikali kutengeneza utaratibu ama sheria ya kuwahakikishia stahiki zao wake na wenza wa viongozi wa juu, akiwemo Rais, mara baada ya wenzi wao kuchaguliwa kushika nafasi hizo.
Mbunge huyo ambaye ni mke wa Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete ameyasema hayo leo Ijumaa Aprili 22,2022 Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia katika makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mwaka 2022/2023.
Amesema wake wa viongozi akiwemo rais, makamu wa rais na Waziri Mkuu mara baada ya wenza wao kushika nafasi hizo wanatakiwa kustaafu na kuendelea na shughuli nyingine.
Amesema kitendo hicho kinamaanisha kuwa utaalamu wake unatoweka.
“Ukiwiwa sana unaweza kusema hebu nianzishe Ngo (mashirika yasiyo ya kiserikali) lakini hata ukianzisha hakuna mtu anayeku suport ni wewe mwenyewe uhangaike ili kuhakikisha unapata raslimali ili uweze kuendesha Ngo,”amesema.
Ameomba Serikali kutengeneza utaratibu wa kisheria ambao mke wa kiongozi anapomaliza muda wake ajue ni nini anachotakiwa kukifanya.
“Ni imani yangu mtatengeneza utaratibu ama sheria inayomuhusu mke wa Rais ama wenza nini bada ya hapo kiendelee kufanyika ni jambo muhimu sana na si kwangu bali ni kwa vizazi vijavyo kujua haki zao,”amesema.
Chanzo: MWANANCHI