Salma Kikwete ataka Sheria ya Stahiki za wake wa Viongozi Wakuu

Salma Kikwete ataka Sheria ya Stahiki za wake wa Viongozi Wakuu

Hicho kitu hakiwezekani, tunaweza pata rais akamuoa dada yake ili apate stahiki au rais akamroga mke mkubwa ili arithi stahiki. Ni kama ilivyo kwa makamu wa rais kwa sasa ktk katiba, ni rahisi sana makamu wa rais kumuua rais ili awe rais kama ilivyotokea kwa Dkt Magufuli
Mkuu unataka kusema nini?😂😂
 
Kitu kimoja ambacho watanzania wengi hawafahamu ni kwamba hawa wanaojitambulisha kuwa wenye chama ama wenye nchi wanatamani wajirithishe uongozi na rasilimali za nchi vizazi na vizazi.Wanatamani wapewe hakimiliki ya teuzi,chaguzi na rasimali.

Kama kazi ambazo walifanya walilipwa na kuchuma na mpaka leo serikali inawajengea nyumba na kuwapa magari ya kifahari hawaridhiki tu.

Hilo kundi la walamba asali hakuna hata mmoja anaetoka katika list ya wapigania uhuru ni wapiga dili tu hawana uchungu na nchi hii
 
Aisee ...! hicho ndicho wananchi wa Mchinga walimtuma akawasemee Bungeni?
Huko Mchinga kuna Changamoto kibao yeye hazioni.?
Hawa wote hawakwenda bungeni kihalali, kwa nguvu ya wananchi, hivyo hawezi kukumbuka wananchi. Na haya ndiyo matokeo ya kuwa na kiongozi mkuu wa nchi mwenye upeo mfupi. Wabunge wanatetea matumbo yao na wengine kufikia hatua ya ku-suggest wananchi wenye nchi wapelekewe vifaru vya kijeshi viwashughulikie.
 
Labda ukute alikua anamlenga mama Janet asaidiwe huenda Serikali imemtupa Ila nawaza tu but sidhan kama ilikua sahihi?
Aisee mawazo yako yako fyongo kweli kweli. Ndiyo maana CCM inazidi kudharau wananchi kwani wengi hawajitambui. Huyu mama inasemekana (sina uhakika) alileta vi-deal vya kuingiza vitu anavyodai ni vya NGO yake kiholela wakati wa mwendazake lakini akawakiwa kweli kweli na mwendazake kwa kutaka asilipe kodi na wakakosana pakubwa. Naona sasa ule msemo wa paka akitoka.....unajihidhirisha.
 
Hawa watu kama hawakushiba miaka ya mume naibu waziri nishati miaka 4,waziri nje miaka 10, urais miaka 10 pamoja na stahiki zote na JPM akamzawadia ubunge wa kuteuliwa 2016.2020 akalamba ubunge mwengine bado tu anadai chenji?

Na usikute 2025 anapanga foleni na walalahoi kugombea tena.

Eeh Mola tutee waja wako wa Tanganyika
 
Haya mambo ya wekwe kisheria ni muhimu kuliko kusubiria fadhila za aliyeko madarakani. Kwanza ni udhalilishaji wa Viongozi wastaafu.

Lakini mume wa kiongozi anaweza akanyanyapaliwa kama kaoa wake wenza wengine na stahiki za hao wake wenza zikiwa haziko kisheria.
 
Back
Top Bottom