Salma Kikwete ataka Sheria ya Stahiki za wake wa Viongozi Wakuu

Salma Kikwete ataka Sheria ya Stahiki za wake wa Viongozi Wakuu

Habari!
Hii taarifa imenipata nikaona niilete kama ilivyo.

My Take: Yani wanataka kila kitu serikali iwaandalie yani hadi Future yao kweli?

Mbunge wa Mchinga (CCM), Salma Kikwete ameishauri Serikali kutengeneza utaratibu ama sheria ya kuwahakikishia stahiki zao wake na wenza wa viongozi wa juu, akiwemo Rais, mara baada ya wenzi wao kuchaguliwa kushika nafasi hizo.

Mbunge huyo ambaye ni mke wa Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete ameyasema hayo leo Ijumaa Aprili 22,2022 Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia katika makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mwaka 2022/2023.

Amesema wake wa viongozi akiwemo rais, makamu wa rais na Waziri Mkuu mara baada ya wenza wao kushika nafasi hizo wanatakiwa kustaafu na kuendelea na shughuli nyingine.

Amesema kitendo hicho kinamaanisha kuwa utaalamu wake unatoweka.

“Ukiwiwa sana unaweza kusema hebu nianzishe Ngo (mashirika yasiyo ya kiserikali) lakini hata ukianzisha hakuna mtu anayeku suport ni wewe mwenyewe uhangaike ili kuhakikisha unapata raslimali ili uweze kuendesha Ngo,”amesema.

Ameomba Serikali kutengeneza utaratibu wa kisheria ambao mke wa kiongozi anapomaliza muda wake ajue ni nini anachotakiwa kukifanya.

“Ni imani yangu mtatengeneza utaratibu ama sheria inayomuhusu mke wa Rais ama wenza nini bada ya hapo kiendelee kufanyika ni jambo muhimu sana na si kwangu bali ni kwa vizazi vijavyo kujua haki zao,”amesema.

Chanzo: MWANANCHI
Duuh! Sasa mama Salma Kikwete anataka apate mafao kwa kulala na Jakaya Kikwete!

Kwa kweli Tanzania kama nchi tumekwisha na hawa viwavi!
 
Aisee ...! hicho ndicho wananchi wa Mchinga walimtuma akawasemee Bungeni?
Huko Mchinga kuna Changamoto kibao yeye hazioni.?
Hii familia inajisahau. Tanzania ni kubwa na ina watu wengi. Urais ni favour ya Mwenyezi Mungu. Sio ufalme. Tuache kutaka kula na kuvimbiwa kama Tanzania ina familia moja au mbili tu. Tanzania ina watu zaidi ya mil 60
 
Sijaona ubaya ya aliyoyasema, lakini sijui watu wamechukulia kwa mtazamo upi.

Kawaida mtu ukistaafu lazima ulipwe mafao yako.

Mfano Mama janeth alikuwa mwalimu lakini baada ya Magufuli kuwa raisi yeye anastaafishwa kazi. Sasa kwanini asilipwe mafao yake kama mwalimu.

Si yeye amejimaanisha bali hata hao wajao wengine watanufaika
 
Duuh! Sasa mama Salma Kikwete anataka apate mafao kwa kulala na Jakaya Kikwete!

Kwa kweli Tanzania kama nchi tumekwisha na hawa viwavi!
Sio mafao ya kuwa mke wa raisi ila mafao ya kazi yake aliyokuwa akifanya hapo awali
 
Wote wanatunzwa na Serikali hawana shida huyu kuna wakati wa kampeni kumkampenia ubunge salma Kikwete mzee Kikwete alisema kuna vijimaneno wanasema ohh Kikwete kamuacha Salma akacheka niko naye namfanyia kampeni

Salma hayo aliyoongea naona kama kweli kaachika anaongea kwa hasira za kuachika!!

Swala kama hilo haikutakiwa kuongea bungeni simu ya Mama Samia anayo na hata angeweza ongea naye direct nyumbani wakisukana nywele na mama Samia na angempa jibu
Kuongelea bungeni kuna kitu

Kikwete unalo
Duh.
 
Sijaona ubaya ya aliyoyasema, lakini sijui watu wamechukulia kwa mtazamo upi.

Kawaida mtu ukistaafu lazima ulipwe mafao yako.

Mfano Mama janeth alikuwa mwalimu lakini baada ya Magufuli kuwa raisi yeye anastaafishwa kazi. Sasa kwanini asilipwe mafao yake kama mwalimu.

Si yeye amejimaanisha bali hata hao wajao wengine watanufaika
Mkuu umesoma vizuri kweli?
 
Back
Top Bottom