Salma Kikwete: Kutokana na kwamba Waziri mkuu mstaafu Kassim Majaliwa hakutimiza ahadi aliyotuahidi ya kutujengea barabara ya lami ya urefu wa kilomita 4.5 watu wa jimbo la Mchinga, nini mkakati wa Serikali kujenga barabara hiyo ambayo mpaka sasa haijajengwa hata kilomita 0.5?
Serikali: Kwanza nimpongeze sana Salma Kikwete kwa kazi kubwa ya kuwasemea wananchi wa jimbo la Mchinga, Naomba nimuhahakikishie mbune kwamba ahadi za viongozi wetu wa kitaifa ni kipaumbele katika bajeti zetu, na tayari tunatambua kwamba kuna ahadi ya barabara kiwango cha lami katika kata ya Milola kilomita 4.5 naomba nikuhahakishie tayari serikali inaendelea na taratibu za kupata fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo kwa awamu ili kutimiza ahadi ya Waziri Mkuu mstaafu lakini pia ikiwa ni dhamira ya serikali inayoongozwa na Samia Suluhu Hassan.