ChanjoSugu
Member
- Oct 22, 2021
- 14
- 33
Leo tarehe 13 Oktoba 2022, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekamata shehena ya mizigo ya vitenge ya marobota 290 katika kontena mbili yenye thamani zaidi ya tsh. Billioni 5 iliyopitishwa kwa magendo katika bandari zetu.
Mfanyabiashara mwenye shehena hiyo alitorokea Dubai majuma matatu yaliyopita, huku TRA wakiweka doria na ulinzi mkali sana.
Mfanyabiashara huyo wa Kariakoo, mtaa wa Aggrey, Bi. Salome Mgaya, maarufu kama 'Mama Kibonge' au 'Mkinga' amekuwa akifanya jambo lolote bila kuguswa na yoyote pindi anapoingiza mizigo yake nchini kwa njia za magendo. Muda mwingine amekuwa anawatishia watumishi wa Bandari au TRA kuhamishwa au kufukuzwa kazi.
TRA wameendesha Operesheni Maalum chini ya Waziri wa Fedha Mwigulu Madelu Nchemba na kuweza kumdhibiti Mama Kibonge.
Mama Kibonge amekuwa akidaiwa kutamba kwa zaidi ya miaka kadhaa bila kukamatwa na kuguswa na mamlaka nchini Tanzania.
Kwa wasiofahamu na wanaomtetea Mama Kibonge kukamatwa kwa Mizigo yake hawajui kuwa, wanamtetea mkwepaji kodi, fiisadi na haramia wa Mapato ya Nchi yetu.