Mmmh🤔🤔
Sikutarajia kabisa kuwa huyu Mzanzibari angeweza kugeuka na kuwa mpumbavu kiasi hiki..
Kama huyu aliweza kujiapiza kuwa, atakuwepo CHADEMA hata iweje, hii U-TURN sio ya kawaida hata kidogo...
Sasa hakuna shaka yoyote kuwa, Freeman Mbowe yumo nyuma ya mkakati huu. Haiwezekani hawa kina John Mrema, Salumu Mwalimu na Benson Kigaila waliokuwa right hands wake wanafanya ujinga huu bila kupata baraka zake...!
Kwa mwenendo huu, kwa hakika sitashangaa na pengine si muda mrefu na yeye Freeman Mbowe atavikana viapo vyake vya miaka mingi alivyokuwa akiapa majukwaani kuwa "atailinda CHADEMA aliyoijenga kwa jasho na damu hadi tone la damu yake ya mwisho" kwa kuichoma moto nyumba (CHADEMA) aliyoijenga mwenyewe kwa gharama zake na kisha kukimbilia kwenda kuishi kwenye pori linaloitwalo CCM...!!!
Duuh, 🤔🤔🤔 kumbe yaweza kuwa ni kweli kuwa, politics is dirty game..