John Wicks Mulholland
JF-Expert Member
- Apr 13, 2023
- 7,945
- 17,286
Aliye kuwa Naibu Katibu mkuu CHADEMA Salum Mwalim Baada ya kutangaza kukiacha chama chake cha CHADEMA amefunguka mengi huku akisema Uchaguzi wa CHADEMA ulikuwa na uongo mwingi sana, rafu zilikuwa nyingi na siasa chafu jambo ambalo lilotia doa sana.
Soma Pia: Baadhi ya G-55 wakiwemo Benson Kigaila, John Mrema, Catherine Ruge na Salum Mwalimu wajiondoa CHADEMA
Watu kuhama katika Vyama vya Siasa au kuhama Dhehebu la Dini ni jambo la kawaida kabisa hapa duniani. Wala siyo Kitu Kigeni.
Isipokuwa kwa jinsi Mimi ninavyofahamu, nchini Tanzania kuna Makundi Matatu (3) ya Vyama vya Siasa, makundi hayo ni:-
1. Vyama Tawala.
Kwa Sasa kipo kimoja tu, yaani CCM. CCM inatawala nchi hii ikiwa Chama pekee, haijaingia Mseto na Chama kingine chocolate kile Cha Siasa ili kuunda Serikali.
2. Vyama vya Upinzani.
Hivi ni Vyma mbadala ambavyo vinakinzana na Chama Tawala kwa kutumia nguvu za hoja, hoja za nguvu, ushawishi wake katika jamii, n.k. Mainly, Vyama hivi vinalenga hasa masuala ya HAKI na Demokrasia.
3. Vyama Mamluki.
Hivi ni Mkusanyiko wa Vyama ambavyo Vinamilikiwa na Chama Tawala kilichopo Madarakani. Kazi yake kuu ni kufanya Siasa za Geresha, Maigizo, hadaa na Ghiriba ili kuhujumu harakati halali za Kupigania HAKI na Demokrasia katika nchi. Vyama hivi ni Kama vile 'Undercover Agents,' wanaofanya kazi chini ya Mwavuli wa Siasa, lakini nyuma ya pazia vinaifanyia kazi Utawala uliopo na Chama Tawala.