Salum Mwalimu ajiuzulu kwa muda CHAUMMA kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili

Salum Mwalimu ajiuzulu kwa muda CHAUMMA kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili

Jamai Jamii Forum imefungiwa tena?
Maana naona jioni hii kwangu siipati bila VPN.
 
Chadema wangekuwa na moto huo huo kwa CCM kama walivyo kwa Chaumma, Lissu angeisha achiwa.

Amandla...
 

Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu, ametangaza kujiondoa kwa muda katika majukumu yake ya ofisi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zilizowasilishwa dhidi yake mbele ya Kamati Kuu ya chama hicho.​

Hata hivyo, hatua ya Katibu Mkuu huyo kujiondoa kwa hiari katika majukumu yake kwa muda inaonekana kuwa sehemu ya jitihada za kuruhusu mchakato wa uchunguzi kufanyika bila kuathiri utendaji wa chama.
Umasikini wa roho,ni ugonjwa mkubwa sana na mbaya sana kwa hivi vyama masikini!. Kosa la Salum Mwalimu ni,baada ya kupewa gari VXR ya serikali wakati wa uchaguzi,baada ya uchaguzi,aliendelea kuonekana na VXR sasa anaendesha mwenyewe!,kwanza walimtuhumu kuiba gari la tume,walipogindua kuwa ni lake,wanataka maelezo kapata wapi fedha wakati Chauma ni apeche alolo,wanadhani ni fedha za chama chao Salum kawaibia
View: https://youtu.be/pKurLGCz14Y?si=TeE2xh2x1IgCnrWt ,kumbe kainunua kwa pesa yake ya mfukoni!

P
 
Imagine alipewa begi la mipesa lakini bado anasema anakidai chama. So kwa maana nyingine zile pesa za kwenye begi alikuwa anawapa wenzake now anazidai. Hizi ndo mbinu alizokuwa anafanya Mbowe.
Kimsingi baada ya Mbowe kugoma kwends chaubwabwa ambapo project iliandaliwa yeye ndio awe mgombea urais akachomoka hatua za mwisho kabisa hivyo option pekee waliyobaki nayo waliona Salum Mwalim ndio mwenye ushawishi kuliko matapeli wote walioandaliwa kuhama hivyo begi lote la pesa na script ya project alisimamia yeye mwisho wa siku akaishia kuona humo humo kwenye project.
 
Hata chadema mlikuwa na mambo ya kijinga kama haya.

Mnajifanya kumkandia huyo mwenzenu ila mlikuwa mnapigana mpaka matofali.
 
Drug dealers wakizimana hakuna formal conflict resolution. Wanamalizana kimya kimya. Nashangaa hawa mazafakas wanapiga kelele!😁
Hawawezi kumfanya kitu chochote zaidi ya walichokifanya so far (kubweka) tu. Kwasababu huo ulaji alioufanya una back up ya wafadhili wa chama. Hao wanaobweka nao watatishwa na mfadhili wa chama watakaa kimya soon. Wajinga ndio waliwao.
 
Project imefeli vibaya!
Imefaulu. Project ilikua ni ya muda mfupi kwa ajili ya kudhoofisha Chadema na kuionyesha dunia kwamba Tanzania ni nchi ya kidemokrasia kuelekea uchaguzi. Mpango wa upigaji umekamilka. Salum na watu wake waliomteua kushika hizo pesa wameshapiga pesa. Mission accomplished.
 

Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu, ametangaza kujiondoa kwa muda katika majukumu yake ya ofisi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zilizowasilishwa dhidi yake mbele ya Kamati Kuu ya chama hicho.​


Soma pia: Sekretarieti ya CHAUMMA Yawasilisha Waraka wa Kutokuwa na Imani na Salum Mwalimu

Katika barua aliyomwandikia Mwenyekiti wa Taifa wa CHAUMMA, Hashim Rungwe, Jumanne Juni 30, 2026, Mwalimu amesema uamuzi huo unalenga kutoa nafasi kwa uchunguzi huru kufuatia tuhuma zilizojadiliwa katika kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Juni 29, 2026, katika makao makuu ya chama hicho, Kinondoni Biafra, jijini Dar es Salaam.


Katika barua hiyo, Mwalimu amesema yuko tayari kushirikiana kikamilifu na timu yoyote ya uchunguzi itakayoundwa na uongozi wa chama, pamoja na kutoa maelezo kuhusu hoja zote zilizotolewa dhidi yake.
Mwalimu, ambaye alikuwa mgombea urais wa CHAUMMA katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, pia amependekeza kuwa katika kipindi chote atakachokuwa nje ya ofisi, majukumu ya Katibu Mkuu yakaimwe na Naibu Katibu Mkuu wa CHAUMMA Tanzania Bara, Benson Kigaila.

Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya kikao cha Kamati Kuu cha chama hicho kugeuka kuwa uwanja wa mvutano, ambapo baadhi ya wajumbe walieleza kutokuwa na imani na Katibu Mkuu huyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vya ndani ya chama, wajumbe wanane kati ya 10 wa Kamati Kuu waliwasilisha waraka wakieleza kutokuwa na imani na Mwalimu, wakimtuhumu kwa kile walichodai kuwa ni matumizi yasiyo na uwazi ya fedha za chama, matumizi mabaya ya madaraka pamoja na ukiukwaji wa misingi ya uongozi.

Vyanzo hivyo vilidai kuwa wajumbe hao wanamtuhumu Mwalimu kwa kushindwa kuweka wazi mapato na matumizi ya chama, kufanya maamuzi makubwa bila kushirikisha viongozi wenzake na kukiendesha chama kwa namna inayodaiwa kukiuka taratibu na kanuni za chama.

Aidha, madai mengine yaliyowasilishwa mbele ya Kamati Kuu ni kwamba Mwalimu amekuwa akidai kuwa anakidai chama fedha alizodai kukitumia tangu alipojiunga nacho mwaka 2025, jambo ambalo limezua sintofahamu miongoni mwa baadhi ya viongozi.

Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani ya chama, kikao hicho awali kilikuwa kimeitishwa kujaza nafasi za wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa CHAUMMA kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa. Hata hivyo, ajenda hiyo ilibadilika baada ya baadhi ya wajumbe kuibua hoja ya kutokuwa na imani na Katibu Mkuu.

Vyanzo hivyo vinaeleza kuwa wengi wa waliounga mkono waraka huo ni viongozi waliohamia CHAUMMA mwezi Mei 2025 wakitokea CHADEMA.

Salum Mwalimu alijiunga na CHAUMMA pamoja na kundi la viongozi wa zamani wa CHADEMA, akiwemo Devotha Minja, Benson Kigaila na John Mrema. Baada ya kujiunga na chama hicho, Mwalimu aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu, akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Mohammed Masoud Rashid, ambaye alihamishiwa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.

Hadi kufikia Jumanne Juni 30, 2026, uongozi wa CHAUMMA haukuwa umetoa taarifa rasmi kuhusu maamuzi ya Kamati Kuu juu ya tuhuma hizo, wala kuthibitisha kuundwa kwa timu ya uchunguzi iliyoombwa na Mwalimu. Hata hivyo, hatua ya Katibu Mkuu huyo kujiondoa kwa hiari katika majukumu yake kwa muda inaonekana kuwa sehemu ya jitihada za kuruhusu mchakato wa uchunguzi kufanyika bila kuathiri utendaji wa chama.
Waache hao chawa na vibaraka wa CCM wauane
 
Umasikini wa roho,ni ugonjwa mkubwa sana na mbaya sana kwa hivi vyama masikini!. Kosa la Salum Mwalimu ni,baada ya kupewa gari VXR ya serikali wakati wa uchaguzi,baada ya uchaguzi,aliendelea kuonekana na VXR sasa anaendesha mwenyewe!,kwanza walimtuhumu kuiba gari la tume,walipogindua kuwa ni lake,wanataka maelezo kapata wapi fedha wakati Chauma ni apeche alolo,wanadhani ni fedha za chama chao Salum kawaibia
View: https://youtu.be/pKurLGCz14Y?si=TeE2xh2x1IgCnrWt ,kumbe kainunua kwa pesa yake ya mfukoni!

P

Wameshamtimua sasa
 
Vipi kuhusu Kada na Mwanachama Mtiifu YERIKO NYERERE??Maana alikuwa anaunga Mkono matumizi mabaya ya gari la Chama yaliyokuwa yanafanywa na Katibu Mkuu Salimu Mwalimu na Muhasibu Mkuu Moza...walipata nalo ajali usiku wa manane huko Morocco-Kinondoni ,YERIKO NYERERE ali post Picha na Video nyingi Mitandaoni akitoa pole kedekede na kuwasifia kwamba wanajenga Chama kwa kujitoa sana??!!!
Basil Lema nimemsoma Mwananchi kule analalamika Salumu amejimilikisha gari ambalo lilitolewa kwa Chama na INEC kwenye Kampeni za Uraisi-2025?!!!
 
Imefaulu. Project ilikua ni ya muda mfupi kwa ajili ya kudhoofisha Chadema na kuionyesha dunia kwamba Tanzania ni nchi ya kidemokrasia kuelekea uchaguzi. Mpango wa upigaji umekamilka. Salum na watu wake waliomteua kushika hizo pesa wameshapiga pesa. Mission accomplished.
Project imefeli kabisa. Nadhani October 29 ilibadilisha Kila kitu.
 
Vijana wa Mbowe ukanjanja kama Mzee wao tu.😀
 
Nyani anamkaimisha Tumbili Ofisi ili Tumbili aunde kamati ya Ngedere kumchunguza Nyani!!
 
Back
Top Bottom