Salum Mwalimu ajiuzulu kwa muda CHAUMMA kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili

Project imefeli kabisa. Nadhani October 29 ilibadilisha Kila kitu.
Salum Mwalimu na kundi lake walienda Chauma kwasababu ya pesa waliokua wameahidiwa kukutana nayo huko. Yeye na wenzake wachache wamepiga hiyo pesa kwa kushirikiana na haohao CCM. Waliokosa mgao ndo hao wanatapatapa na hakuna kitu watafanya. CCM hawana hasara kwasababu wana uwezo kupitia vyanzo vyao vingi vya kifisadi kufidia pesa waliyoipeleka Chauma. Wahanga ktk hili ni wananchi ambao kodi yao na rasilimali zao nyingine za nchi zinatumika kwenye miradi ya kisiasa ya kijinga kama hii. Sisi wananchi ndo tumefeli kwa mara nyingine tena.
 
WAHUNI WA CHADEM MMOJA MMOJA WANAAIBIKA HAHAHA MSIGWA OYEE
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu, ametangaza kujiondoa kwa muda katika majukumu yake ya ofisi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zilizowasilishwa dhidi yake mbele ya Kamati Kuu ya chama hicho.​

Soma pia: Sekretarieti ya CHAUMMA Yawasilisha Waraka wa Kutokuwa na Imani na Salum Mwalimu

Katika barua aliyomwandikia Mwenyekiti wa Taifa wa CHAUMMA, Hashim Rungwe, Jumanne Juni 30, 2026, Mwalimu amesema uamuzi huo unalenga kutoa nafasi kwa uchunguzi huru kufuatia tuhuma zilizojadiliwa katika kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Juni 29, 2026, katika makao makuu ya chama hicho, Kinondoni Biafra, jijini Dar es Salaam.

Katika barua hiyo, Mwalimu amesema yuko tayari kushirikiana kikamilifu na timu yoyote ya uchunguzi itakayoundwa na uongozi wa chama, pamoja na kutoa maelezo kuhusu hoja zote zilizotolewa dhidi yake.
Mwalimu, ambaye alikuwa mgombea urais wa CHAUMMA katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, pia amependekeza kuwa katika kipindi chote atakachokuwa nje ya ofisi, majukumu ya Katibu Mkuu yakaimwe na Naibu Katibu Mkuu wa CHAUMMA Tanzania Bara, Benson Kigaila.

Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya kikao cha Kamati Kuu cha chama hicho kugeuka kuwa uwanja wa mvutano, ambapo baadhi ya wajumbe walieleza kutokuwa na imani na Katibu Mkuu huyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vya ndani ya chama, wajumbe wanane kati ya 10 wa Kamati Kuu waliwasilisha waraka wakieleza kutokuwa na imani na Mwalimu, wakimtuhumu kwa kile walichodai kuwa ni matumizi yasiyo na uwazi ya fedha za chama, matumizi mabaya ya madaraka pamoja na ukiukwaji wa misingi ya uongozi.

Vyanzo hivyo vilidai kuwa wajumbe hao wanamtuhumu Mwalimu kwa kushindwa kuweka wazi mapato na matumizi ya chama, kufanya maamuzi makubwa bila kushirikisha viongozi wenzake na kukiendesha chama kwa namna inayodaiwa kukiuka taratibu na kanuni za chama.

Aidha, madai mengine yaliyowasilishwa mbele ya Kamati Kuu ni kwamba Mwalimu amekuwa akidai kuwa anakidai chama fedha alizodai kukitumia tangu alipojiunga nacho mwaka 2025, jambo ambalo limezua sintofahamu miongoni mwa baadhi ya viongozi.

Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani ya chama, kikao hicho awali kilikuwa kimeitishwa kujaza nafasi za wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa CHAUMMA kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa. Hata hivyo, ajenda hiyo ilibadilika baada ya baadhi ya wajumbe kuibua hoja ya kutokuwa na imani na Katibu Mkuu.

Vyanzo hivyo vinaeleza kuwa wengi wa waliounga mkono waraka huo ni viongozi waliohamia CHAUMMA mwezi Mei 2025 wakitokea CHADEMA.

Salum Mwalimu alijiunga na CHAUMMA pamoja na kundi la viongozi wa zamani wa CHADEMA, akiwemo Devotha Minja, Benson Kigaila na John Mrema. Baada ya kujiunga na chama hicho, Mwalimu aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu, akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Mohammed Masoud Rashid, ambaye alihamishiwa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.

Hadi kufikia Jumanne Juni 30, 2026, uongozi wa CHAUMMA haukuwa umetoa taarifa rasmi kuhusu maamuzi ya Kamati Kuu juu ya tuhuma hizo, wala kuthibitisha kuundwa kwa timu ya uchunguzi iliyoombwa na Mwalimu. Hata hivyo, hatua ya Katibu Mkuu huyo kujiondoa kwa hiari katika majukumu yake kwa muda inaonekana kuwa sehemu ya jitihada za kuruhusu mchakato wa uchunguzi kufanyika bila kuathiri utendaji wa chama.
TAPELI LA CHADEMA MNALIPA MAMLAKA SHOEWINE WOTE

WAFU WAZIKE WAFU WAO PLS

MKOME NA MTUACHE TUNA JAMBO LETU
 
Huyu mshenzi ana akili kama za babake alizodai anaidai chadema 😆 😂 😆 😂 😆 😂 😆 😂 😆 nyooozake
 
Huyu jamaa nikimuona tu, najihisi kutapika, hana tofauti na kina Msigwa, Sumaye, Dr Slaa, Marehemu Lowassa, Marehemu Membe n.k Malaya wa kisiasa hao, wasiojua wanapigania nini. Kwa Zanzibar role model wake ni marehemu Maalim, alizaliwa CCM, akakulia CUF na kufia ACT Wazalendo.
Katika orodha yako hiyo muondoe DK.Slaa.
Hana sofa za umalaya was kisiasa.
 
Huyu ana kadi ya CCM way before hajaenda Chadema, baadae akapewa ubalozi wa CCM hao hao na akarudi kuuchukua, this time yupo Chaddema. So Unstable.
 
Hii inaweza ikawa ajenda ya kujaribu kututoa kwenye mambo ya maana au ni njia ambayo wanataka kuendea CDM
Hili swala nililiona, sasa zimeanza chokochoka za akina yericko na akina mchome
 
Back
Top Bottom