Salva Rweyemamu wa IKULU yuko wapi?

Salva Rweyemamu wa IKULU yuko wapi?

Status
Not open for further replies.

Halisi

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2007
Posts
2,802
Reaction score
614
Wakuu naomba munisaidie, nimekutana na hii taarifa ikiwa na "Kaimu Mkurugenzi"... kaka yetu Salva yuko wapi? Nafahamu hata anapokuwa safari na Rais huko huko aliko huwa anatoa taarifa na hakuna Kaimu, leo kulikoni? Au ndio LAPTOP inawasumbua? Labda kaenda kuitafuta.

MODE IKIISHA MUDA AU KUPATA MAJIBU MWAFAKA UNAWEZA KUIONDOA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail : press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tumeona ni vizuri kuwashirikisha katika tukio hili la kuwakabidhi viongozi wa chama cha Maalbino Tanzania jezi zilizotolewa na Mheshimiwa Rais.

Mtakumbuka tarehe 19 Oktoba, 2008 wakati Rais alipopokea maandamano ya kulaani mauaji ya maalbino, pamoja na mambo mengine aliahidi kutoa jezi na vifaa vingine vya michezo kwa timu ya maalbino itakayocheza mechi ya kirafiki na waheshimiwa wabunge leo tarehe 26 Oktoba, 2008 katika uwanja wa taifa.

Vyombo vya habari vimekuwa ni wadau na washiriki wakubwa katika kufichua vitendo vya ukatili na unyayapaa wanavyofanyiwa maalbino. Mheshimiwa Rais anazidi kuwapongeza kwa juhudi zenu katika kipigania haki za maalbino.

Rai yetu ni kwamba tunaomba kwa pamoja tuendeleze ujumbe kwamba maalbino ni binadamu kama walivyo binadamu wengine wanaopaswa kuheshimiwa na kupata haki zote na fursa ya kushiriki katika shughuli zote za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Hii ndiyo maana Mheshimiwa Rais ameamua kutoa jezi 33 na vifaa vinavyohusiana na michezo vyenye thamani ya Shilingi Milioni Mbili Laki Moja Arobaini na Tatu Elfu (Shs. 2,143,00/=) kwa maalibino ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu mechi ya leo kati yao na waheshimiwa wabunge.

Ahsanteni sana.

Kisare Makori,
Kaimu Mkurugenzi,
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais – Ikulu,
DAR ES SALAAM.

26 Oktoba, 2008
 
Attachments

Wakuu naomba munisaidie, nimekutana na hii taarifa ikiwa na "Kaimu Mkurugenzi"... kaka yetu Salva yuko wapi? Nafahamu hata anapokuwa safari na Rais huko huko aliko huwa anatoa taarifa na hakuna Kaimu, leo kulikoni? Au ndio LAPTOP inawasumbua? Labda kaenda kuitafuta.

MODE IKIISHA MUDA AU KUPATA MAJIBU MWAFAKA UNAWEZA KUIONDOA

Huyu Kisare Makori, ni wa kule Tarime!!!!! (Joke)
 
Labda na e "kapotea" kama "ilivyopotea" laptop!
 
Hii ni taarifa ya issue ndogo sana hapo ikulu hata kama Salva yupo, sio lazima kila taarifa asaini yeye ndio maana ana wasaidizi. Siku ukiona rais anatoa zawadi za Iddi kwa watoto yatima na ukaona anakabidhi zawadi hizo siku zote ni Mninukulu wa Ikulu, Jee utauliza rais yuko wapi?.
Salva hebu endelea kujipumzikia leo ni week end. Kesho endelea na kuchapa kazi nzuri kwa ujenzi wa taifa katika utaratibu wako uliojipangia, ila pia ukiamua unaweza kutoa kijistatement cha by the way kujulisha laptop ulikuwa nayo wewe hivyo haijapotea there will be no ambarassment.
 
Kweli kabisa Mkuu Pasco,wanamsumbua sana mheshimiwa Salva wakati anatakiwa kuwa kwenye mapumziko. Hata hilo la laptop ni suala dogo sana, wala hastahili kuhangaisha akili yake kwa ajili ya hilo, aendelee kupumzika tu
 
Hii ni taarifa ya issue ndogo sana hapo ikulu hata kama Salva yupo, sio lazima kila taarifa asaini yeye ndio maana ana wasaidizi. Siku ukiona rais anatoa zawadi za Iddi kwa watoto yatima na ukaona anakabidhi zawadi hizo siku zote ni Mninukulu wa Ikulu, Jee utauliza rais yuko wapi?.
Salva hebu endelea kujipumzikia leo ni week end. Kesho endelea na kuchapa kazi nzuri kwa ujenzi wa taifa katika utaratibu wako uliojipangia, ila pia ukiamua unaweza kutoa kijistatement cha by the way kujulisha laptop ulikuwa nayo wewe hivyo haijapotea there will be no ambarassment.

Kuna tofauti kubwa mtu anaposaini taarifa kwa wadhifa wa "Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano" na anaposaini "kwa niaba ya" au k.n.y.

Ukitumia wadhifa wa "Kaimu" maana yake ni kwamba yule bosi mwenyewe hayupo ofisini kwa sababu labda yuko likizo au kasafiri, hivyo nafai yake imeshikiliwa na mtu mwingine. "Kwa niaba ya" maana yake ni kwamba bosi yupo lakini taarifa inaweza kusainiwa na ofisa mwingine mwenye mamlaka ya kufanya hivyo kwa mujibu wa taratibu za kiofisi.

Hivyo, kwa case hii, ina maana Salva hayupo, labda yuko safari ya kikazi, likizo au anaumwa na Majukumu yake kapewa ofisa mwingine hadi atakaporejea ofisini.
 
Last edited:
Hii ni taarifa ya issue ndogo sana hapo ikulu hata kama Salva yupo, sio lazima kila taarifa asaini yeye ndio maana ana wasaidizi. Siku ukiona rais anatoa zawadi za Iddi kwa watoto yatima na ukaona anakabidhi zawadi hizo siku zote ni Mninukulu wa Ikulu, Jee utauliza rais yuko wapi?.
Salva hebu endelea kujipumzikia leo ni week end. Kesho endelea na kuchapa kazi nzuri kwa ujenzi wa taifa katika utaratibu wako uliojipangia, ila pia ukiamua unaweza kutoa kijistatement cha by the way kujulisha laptop ulikuwa nayo wewe hivyo haijapotea there will be no ambarassment.

Pasco hujamwelewa Halisi au unachanganya kati ya usaidizi na ukaimu. Labda nikwambie kwamba Afisa wa chini akitoa taarifa kwa niaba ya Afisa mwenye cheo cha juu ataandika k.n.y (kwa niaba ya) au ataandika cheo chake (mfano Mkurugenzi msaidizi/naibu mkurugenzi etc), huwezi kukaimu nafasi ya mtu kama yupo ofisini.
 
Hapa mtaletwa Kiswahili:

Naibu wa
Kaimu wa
Kwa niaba ya ...

All in all, nimesoma taarifa yenyewe na nimeshangaa kuona juhudi za Rais kupambana na mauaji ya Albino!!
 
''Vyombo vya habari vimekuwa ni wadau na washiriki wakubwa katika kufichua vitendo vya ukatili na unyayapaa wanavyofanyiwa maalbino. Mheshimiwa Rais anazidi kuwapongeza kwa juhudi zenu katika kipigania haki za maalbino.''

Idiocracy at its best!
I guess mapigano dhidi ya ufisadi are not worth the attention.
Kubenea and crew,ona sasa mmekosa jezi kwa kupigania vijimambo vidooogo.
 
hivi kuna mtu anaye edit hizo taarifa au?........
 
Salva ameonekana Afrika Kusini, wanarejea leo usiku....
 
Inamaana ni kosa msaidizi wa Salva kufanya kazi za Salva au tunataka yeye kila siku akae ofisini?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom