Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 614
Wakuu naomba munisaidie, nimekutana na hii taarifa ikiwa na "Kaimu Mkurugenzi"... kaka yetu Salva yuko wapi? Nafahamu hata anapokuwa safari na Rais huko huko aliko huwa anatoa taarifa na hakuna Kaimu, leo kulikoni? Au ndio LAPTOP inawasumbua? Labda kaenda kuitafuta.
MODE IKIISHA MUDA AU KUPATA MAJIBU MWAFAKA UNAWEZA KUIONDOA
MODE IKIISHA MUDA AU KUPATA MAJIBU MWAFAKA UNAWEZA KUIONDOA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail : press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENTS OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tumeona ni vizuri kuwashirikisha katika tukio hili la kuwakabidhi viongozi wa chama cha Maalbino Tanzania jezi zilizotolewa na Mheshimiwa Rais.
Mtakumbuka tarehe 19 Oktoba, 2008 wakati Rais alipopokea maandamano ya kulaani mauaji ya maalbino, pamoja na mambo mengine aliahidi kutoa jezi na vifaa vingine vya michezo kwa timu ya maalbino itakayocheza mechi ya kirafiki na waheshimiwa wabunge leo tarehe 26 Oktoba, 2008 katika uwanja wa taifa.
Vyombo vya habari vimekuwa ni wadau na washiriki wakubwa katika kufichua vitendo vya ukatili na unyayapaa wanavyofanyiwa maalbino. Mheshimiwa Rais anazidi kuwapongeza kwa juhudi zenu katika kipigania haki za maalbino.
Rai yetu ni kwamba tunaomba kwa pamoja tuendeleze ujumbe kwamba maalbino ni binadamu kama walivyo binadamu wengine wanaopaswa kuheshimiwa na kupata haki zote na fursa ya kushiriki katika shughuli zote za kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Hii ndiyo maana Mheshimiwa Rais ameamua kutoa jezi 33 na vifaa vinavyohusiana na michezo vyenye thamani ya Shilingi Milioni Mbili Laki Moja Arobaini na Tatu Elfu (Shs. 2,143,00/=) kwa maalibino ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu mechi ya leo kati yao na waheshimiwa wabunge.
Ahsanteni sana.
Kisare Makori,
Kaimu Mkurugenzi,
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu,
DAR ES SALAAM.
26 Oktoba, 2008