Oluwa ni
JF-Expert Member
- May 24, 2015
- 717
- 445
Nimekuwa nikifuatilia sana hiki kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa kila Ijumaa ya wiki usiku na Sam Misago. Kumekuwa na interview za wasanii mbalimbali lakini nimegundua hiki kipindi ni jipu kwa wasanii wetu!!!
Anachokifanya Sam ni ujinga wa hali ya juu ambao hauwezi kuvumilika! Kama kuna wadau wengine huwa wanafuatilia hiki kipindi mtakuwa mmegundua na kuona nini kinachoendelea!!
FNL ya juzi kama uliona Shetta alikuwa ana interview kwenye hicho kipindi na Sam lakini Sam alionesha kutomkubali kabisa Shetta kutokana na maswali aliyokuwa anamuulizaa! Swala la EATV Awards, Sam alionekana kumkandia sana Shetta na kuonesha waziwazi kuwa katika vipengele alivyopo Shetta ni kama hawezi kuchukua tuzo kwa sababu fulani yupo! SHAME ON U SAM!
Wewe ndiye unayeamua mshindi au kura ndo zinaamua? Na kama mnajua fulani ndo atakuwa mshindi, ya nini kuweka usiku kwanini msimpe Tuzo aendeee? Kwanini kuna mashindano?
Shetta alipoteza kabisa 'mood' juzi kutokana na Sam. Kwa walioona watakuwa mashahidi wa hayaa. Sijui ni kukosaa taaluma ya utangazaji au la, lakini hii sio maara ya kwanza kwa Sam. Nakumbuka kuna siku Harmonize alikuwa na Interview FNL, Sam alikomaa na Swala la Harmonize kumuiga Diamond hadi Harmonize akapanic maana anajibiwa lakini interview nzima ni kama alimuitia kumuuliza hilo swalii!
Sam na FNL yake sio hayoo tu, yapo mengi lakini kwa hili la juzi ni wakati wa wasanii sasa Kukisusia hiki kipindiii kwa alivyofanyiwa Shetta!!! Na kwa maswali yale, ningemuomba Shetta kiutu uzimaa ajitoe kabisa katika kuwania tuzo hizi za AETV awards!! Maana aliabishwa kuwa hawezi shindana na Mwafulani!!!
Sam kama upo hapa na unasoma haya au jamaa ake yeyote wa karibu amfikishie taarifa nafikiri kungekuwa kuna kupiga simu kipindi cha juzi Sam angekoma!! Utangazaji bila taaluma matokeo yake ndo hayo.
Sam misago boya tu huwa ana maswali ya kejeli sana mm huwa namfatlia kama anamhoji msanii ambaye kdg bdo kwny mzk anakuwa na maswal ya kejeli.........
Mshkaj anajiona sana sema shetta hanagi nyng atapotezea tu nakumbuka kuna ck aliwah kumletea jeuri Linex kdgo zingepingwa ngumi........
[HASHTAG]#StepByStep[/HASHTAG]