Samahani kwa Kuuliza hivi Daraja Jipya la Mto Wami limeshazinduliwa? Na kama bado ni Kwanini?

Ina maana huyu bibie hana vision ? Yeye kufubgua nchi na bakuli waarabu na uza uza rasilimali?
 
Kazi yangu Kubwa ni kusoma tu Comments zenu, ila popote pale ulipo Hayati John Pombe Magufuli Roho yako ilale mahala pema peponi. Amen.
Kwani wakati unaenda Lutindi, huwa unapita njia gani? Acha kuchosha watu hapa. Halafu ukumbuke hilo daraja limejengwa kwa fedha zilizotokana na kodi yako.
 
Yawezekana ukawa una elekeza mtu wa miaka ya 2000 hajui nchi China, Japan, Vietnam n.k maendeleo yalikuja vipi? Tena mbaya zaidi kwa mwafrika eti umbembeleze hakuna maendeleo yatakayopatikana hadi mwisho wa dahari.
 
Kwani wakati unaenda Lutindi, huwa unapita njia gani? Acha kuchosha watu hapa. Halafu ukumbuke hilo daraja limejengwa kutokana fedha zilizotokana na kodi yako.
Huko Lutindi huwa naenda na Mamaako.
 
Kwani lisipozinduliwa inakuaje?
Inaonyesha ni jinsi gani tusivyotaka Mambo makubwa na mazuri ya Mwamba Hayati John Pombe Magufuli yaendelee Kujulikana na kila Siku azidi Kukumbukwa tofauti na Waigizaji Filamu wa Pwani ya Bahari ya Hindi.
 
Sahihi, waswahili wanapenda shughuli sana.
Kwao hakuna jambo dogo.
 
Shida ya wananchi haikuwa kuzindua daraja bali kulitumia! Mwisho tenda wema usepe zako siyo unasubiri misifa kama shetani!
Hata sio kutenda wema,sio hisani hiyo.
Ni kuwajibika kodi za raia waliolipia hilo daraja na wanaokutunza kama kiongozi.
 
GENTAMYCINE nitakuwa maradufu yake.
Awapi. Ukitaka kuwajua Watz jaribu kuomba kazi hata ya kujitolea kwa Mtendaji wa Kijiji. Halafu uje hapa uniambie umeona nini.

Kwanza utagundua kwamba washawishi wakubwa wa rushwa ni wananchi wa kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…