Samahani Rais Samia Suluhu Hassan

Samahani Rais Samia Suluhu Hassan

F-Merylin

Senior Member
Joined
Dec 26, 2016
Posts
128
Reaction score
177
Mama Samia

Wengi watatoa maoni yao kuhusu hotuba yako na wahariri wa vyombo vya habari lakini leo sitajiunga nao bali nitakupa zawadi ya kutimiza siku 100 kwa Post hii ya kukuomba msamaha. Sio kwa post zangu ambazo zimekuwa critical bali kwa "Kutokukupa Muda". Mheshimiwa Rais wote walio na mashaka na uongozi wako hawana shida na wewe bali wasiwasi wa kuporomoka kwa mazuri ya awamu ya tano na ya kwanza. Personally nasali kwa ajiri yako kila siku lakini ninaogopa sana kuhusu matokeo ya hatua zinazohusu yafuatayo:

1. Kujaribu kufurahisha taasisi za kimataifa, nchi za magharibi na wawekezaji wa nje. Hawa watu, pamoja na nia yako nzuri wako kimaslahi zaidi na kinyonyaji zaidi. maeelekezo yao na uwekezaji wao unaweza kuwa na manufaa kwetu katika ajira tu na sio kupanda kwa uchumi. wakikupa 20 wanchukua 80. Mradi wa Bagamoyo Port unafikirisha sana! Resources zetu ni zetu kwa ajili ya wote na sio wachache wenye maamuzi.

2. Korona - hakuna siri kuwa kuna mambo mengi yasiyoeleweka katika ugonjwa huu. Chanjo zimewaua wengi na nchi kama India uwepo wa chanjo umeongeza vifo. Lakini pia hivi vifaa vingine vinaambukiza korona zaidi. Leo umesema wagonjwa wako kama 100. utashangaa idadi kupanda baada ya bidii zako (kama chanjo na kuleta masks) kufanyika. Je na wewe utafuata nyayo za wenzako kutangaza idadi kubwa ya wagonjwa ili upata hela zaidi? Everything is a hoax /scum about Covd-19! unataka kuzama huko!

3. Kuombaomba na kukopa na kuwapigia magoti wazungu unashusha 'umaskini jeuri' wetu ambao ulimfanya mtangulizi wako awe maarufu. Siwezi kujisikia vizuri kama Rais akivishwa kilemba cha ukoka kama Abunuasi alivyomsifia mfalme aliyemfanya atembee uchi. Wazungu wanakusifia wakati wanaku-use! Watanzania na umaskini wetu hatupendi kuwa wanyonge kwa mataifa mengine!

4. Upigaji ndani ya serikali - Mama waswahili ni wezi by nature. Ukigeuza tu shingo wataiba na maskini watasahaulika. Hata hiyo mikopo ya halmashauri itaishia nikononi mwa wajanja. kuwa na details ni bora kuliko kuwatumia assistants. Jamaa hakuwa analala...!

Hata hivyo samahani kuwa sijakupa muda. Umefanya mazuri mengi kuliko kuwa na kasoro. Muda utaamua kuwa worries zangu hapo juu ziko justified au hapana. Nakutakia utawala mwema! Kama ulivyoomba nitakupa muda. Mwaka mmoja unakutosha wakati nasali kwa ajili yako!

Nimelize kwa kukutonya. Unasifiwa na wengi lakini mitaani wanaolalamika kuhusu msimamo wako kuhusu Uviko-19 na mengine machache ni wengi pia! Usiwasibie masikio. Urais una mwisho ila legacy njema (kama a watangulizi wako katika yale mazuri) haina mwisho. Na mabaya hayasahauliki pia.
 
Hayo mambo manne ulioyataja hapo juu yanatokana na wewe kuwa Brain washed na mwanakwenda zake. Hayo mambo yote manne mwanakwenda ndio aliharibu sana Mama anajaribu tu kuinua ukuta .....ikitokea ukaanguka tena asilaumiwe yeye bali mtangulizi wake.
 
Hayo mambo manne ulioyataja hapo juu yanatokana na wewe kuwa Brain washed na mwanakwenda zake. Hayo mambo yote manne mwanakwenda ndio aliharibu sana Mama anajaribu tu kuinua ukuta .....ikitokea ukaanguka tena asilaumiwe yeye bali mtangulizi wake.
Hakuna suala la brainwashing hapa. hizo ni facts na weaknesses za utawala wa sasa! tutampa muda!
 
Hakuna suala la brainwashing hapa. hizo ni facts na weaknesses za utawala wa sasa! tutampa muda!
Naungana na huyo aliyekuambia kuwa umekuwa brainwashed.

Naamini ulipumbazwa na maneno mengi ya uwongo na utawala uliotangulia.

Rais afanye kazi kujenga uchumi wa kisasa. Ile primitive thinking ya marehemu ya kufikiria kuwa kila Taifa linataka kuiibia Tanzania, na kuwadanganya Watanzania kuwa tulikiwa tunaibiwa sana halafu akashindwa kumpata mwizi hata mmoja ilimsaidia marehemu kuwa popular kwa wasio na ufahamu lakini haikuwa na msaada wowote kwa Taifa. Ndiyo maana ukuaji wa uchumi wa Taifa letu ulikuwa ukishuka kila leo, lakini marehemu akiwadanganya wajinga kuwa tunapaa kwa kasi, na wajinga wakaamini.
 
Naungana na huyo aliyekuambia kuwa umekuwa brainwashed.
Kila mtu anaweza kusema kama wewe. shida ni uwezo wa kuchambua hoja. Pitia hoja zangu na useme ipi sio sahihi! Upigaji ndani ya serikali? Kuwapigia magoti wazungu na kuwa kibaraka? Au Madhara ya chanjo za korona na mipango nyuma ya pazia katika hili? Yote haya ni facts na historical.
 
Back
Top Bottom