HABARI WANA JAMII FORUM
Nasikia kitaalamu samaki aina ya papa na jamii za samaki wa aina hii huwa wana kiwango kikubwa Cha kemikali ya madini ya mercury na ni hatari kwa afya ya mwanadam
Je swala hili kitaalamu ni Kweli?
Nasikia kitaalamu samaki aina ya papa na jamii za samaki wa aina hii huwa wana kiwango kikubwa Cha kemikali ya madini ya mercury na ni hatari kwa afya ya mwanadam
Je swala hili kitaalamu ni Kweli?
- Tunachokijua
- Papa ni samaki, na wengi wao wana umbo la kawaida la mwili lenye umbo la mviringo na refu. Kama samaki wengine, papa ni ectothermic (wana damu baridi), wanaishi majini, wana mapezi, na wanapumua kwa kutumia mabonde ya hewa (gills).
Hata hivyo, papa wanatofautiana na samaki wa mifupa (Osteichthyes). Tofauti moja ni kwamba mifupa ya papa imetengenezwa kwa cartilage (gamba laini) badala ya mifupa halisi. Tofauti nyingine inayoonekana ni kwamba samaki wa mifupa kwa kawaida huwa na tundu moja la mabonde ya hewa, ilhali spishi zote za papa, isipokuwa mbili, zina matundu matano ya mabonde ya hewa.
Madai
Mdau amehitaji kujua iwapo nyama ya samaki aina ya papa ni hatari kw abinadamu kutokana na kuwa na madini ya zebaki (mercury).
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia madai ya mdau aliyehitaji kupata uhalisia kuhusu hatari ya nyama ya papa kutokana na kuwa na madini aina ya Zebaki(Mercury) na kubaini kuwa ni ya kweli.
JamiiCheck imepitia tafiti na machapisho mbalimbali mathalani tovuti ya Koiko Conservation International imeleza kuwa ni hatari kwa binadamu kula nyama ya papa kwa kuwa ina athari kwa afya. Papa huzalisha kemikali mbalimbali ambazo iwapo zitaingia kwenye mwili wa binadamu zinaweza kuleta madhara tofauti kiafya, miongoni mwa kemikali hizo ni Methlymercury, Lead, Arsenic na Urea. Kemikali hizi zikiingia kwenye mwili wa binadamu zinaweza kuleta athari kwenye moyo, mapafu, ini, figo, ubongo, pia huleta changamoto katika kumbukumbu, kiharusi, saratani ama kifo.
Utafiti uliofanywa na Gelsleichter pamoja na wenzake na kuchapishwa katika jarida la taaluma la Endangared species research kuhusu kiwango cha Zebaki za chuma kwa papa aina ya Oceanic whitetip (Carcharhinus longimanus). Utafiti huo unaeleza kuwa aina hii ya papa ni miongoni mwa papa wakubwa ambao kwa kipindi cha nyuma walikuwa wengi kwa idadi ila kwa hivi sasa wapo katika hatari kubwa ya kupotea. Miongoni mwa sababu zilizotajwa kuwapoteza papa hawa ni kutokana na uwezo wao wa kujilimbikizia kiasi kikubwa cha sumu kutoka kwenye mazingira, jambo linalowaweka katika hatari kubwa kutokana na uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na shughuli za binadamu.
Katika utafiti wao walioufanya kwa papa 26 walibaini kuwa papa hao wana kiwango kikubwa cha Zebaki (Mercury) katika mifupa, misuli, chembechembe nyekundu za damu huku ikonekana mapezi ndiyo yana Zebaki nyingi zaidi. Na wakahitimisha kuwa Zebaki inahatarisha papa aina ya Oceanic Whitetip katika bahari ya Atlantiki ya kaskazini magharibi na vile vile kwa binadamu wanaokula papa wa aina hiyo.
Utafiti mwingine uliofaywa nchini Afrika kusini mwaka 2016 na kisha kuchapishwa katika jarida la kitaaluma la Science of the total environment kuhusu viwango vya Zebaki kwa papa na athari zake kwa afya kutoka pwani ya mashariki ya nchi hiyo, ulibainisha kuwa kumekuwepo na matumizi makubwa ya zebaki ambayo yanapeleka athari kwa papa lakini pia kwa walaji wa nyama ya papa.