Mwanafunzi mtoro
JF-Expert Member
- Aug 3, 2021
- 222
- 806
Wasalaaamu ndugu , jamaa na marafiki wa JF . Haika nawathamini sana.
Kila mmoja wetu amepata kushituka kwa taarifa ya wasomi wetu nguli wa mambo ha mazingira kwa kusema samaki katika mto mara wamekufa kutokana na kinyesi na mikojo ya ng'ombe. Kabla ya kupinga au kuunga mkono majibu ya tafiti zao kwanza tuangalie tafiti zingine kuhusu hilo
Tafiti zinasema hivi
1 Kinyesi cha ng'ombe (organic manure) pamoja na mbolea zingine zinapo ingia majini huchochea ukuaji wa mimea au viumbe hai wadogo wadogo wanaoitwa kwa kiluguru "algae" au "mwani" kwa kizaramo. Ukuaji wa mwani unahitaji hewa ya oxijeni iliyoyeyuka katika maji (disolved oxygen ). Wakati huohuo samaki anahitaji hewa hiyo hiyo ya oxijeni kufanya upumuaji. Hewa ya oxijeni iliyopo katika maji ni ndogo ukilinganisha na iliyopo katika anga hewa(atmosphere ). Katika kupokonyana hewa ya oxijeni kati ya samaki na mwani basi samaki watakosa hewa hiyo na kufa. Mwasho wa siku samaki watakufa na kuelea juu ya maji.
Katika hilo pia kuna mambo mawili ya kuangalia
(a) wingi wa mimea mwani
(b) uchache wa maji, mara nyingi athari hii hutokea kwenye bwawa sehemu ambayo maji yenye hewa chafu hayatoki na yenye hewa safi hayaingii
2 Jambo la pili ni mkojo wa ng'ombe.
Mkojo wa ng'ombe una kiasi kikubwa cha ammonia ambayo ni sumu kwa samaki. Japokuwa hata samaki anaweza kuzalisha ammonia lakini yake ni chache na inawahi kuwa "diluted" na maji. Sumu hii ya ammonia pia ili iweze kuwadhuru samaki lazima mambo mawili yawepo
(a) Uchache wa maji au maji yasiyo na mwingiliano mfano bwawa.
(b)Wingi wa kiasi cha amonia. Kuna kiasi chake cha ujazo wa amonia kinachoweza kuathiri samaki katika uwiano wa amonia na maji.
Tukio kama hili la kufa samaki limewahi kutokea sehemu mbalimbali mfano katika bwawa la Dakota. Nimeambatanisha picha
TURUDI KATIKA MAZINGIRA YA MTO MARA
Kabla ya kuuzungumzia mto mara ambapo mimi binafsi siyajui (tutawaachia wengeji wajadili) kwa udogo tujadili mazingira ya Morogoro ambapo kuna ng'ombe wengi na mabwawa au mito mingi
Kwa uzoefu wangu kuna kipindi cha masika ambapo ngombe hula nyasi ngingi na kunywa maji mengi lakini wanapoenda kuywa maji sijawahi kuwaona samakiwamekufa baada ya siku chache mbele kwa kukosa hewa iwe kwenye mito au hata bwawa dogo lenye samaki kama dagaa,kambale (samaki kiburi) na perege.
Nimesikia ng'ombe wa mara wanatoa kinyesi kilo 20+ na mkojo lita 20+ hakika hii ni bahati sana na wala sitegemei watu wa mara mje kubisha kwakuwa tunaamini majibu ya tafiti hizi wamezipata kwa wafugaji hivyo sisi ambao hatuna hata kuku tunawaacha ninyi wafugaji wa mara na maeneo mengine mlumbane kwa hoja. Hoja yangu mimi hapa ni hii. Tuamini kweli ng'ombe mmoja anatoa kinyesi kilo 20 na mkojo lita 20 lakini wanatoa taka hizo masaa 24 wakiwa mtoni au kandokando ya mto? Jibu bila shaka ni hapana. Ningumu sana ng'ombe kujisaidia kilo 20 na mkojo lita 20 kwenye mto basi kama ni hivyo labda kama watakojoa lita 30 au 35 ili mkojo mwingine atajisaidia zizini. Ng'ombe hawezi kuwa kama binadamu kwamba apaone mtoni ndio chooni akifika amalize shida zake zote kisha aondoke.
Tuwaulize watu wa mto mara ni kweli hapo walipokufa samaki maji yake hayana mwingiliano na maji masafi?
Tuwaulize watu wa karibu na mto mara kuna mwani umeota unaonekana hata kwa uchache?
KAMA VYOTE SIYO NINI INAWEZA KUWA
Sijui hasa ni lini samaki hao walionekana kufa kama nikipindi hiki mvua zimerudi au pale mwezi wa pili. Kama ni mwezi wa pili , kwa maji yasiyo na mwingiliano samaki anaweza kufa kama maji yatapata joto kali. Tuwaulize wakazi wa karibu na mto je hili linawezekana?
Kingine kinachoweza kuwaua samaki ni uvuvi haramu. Zipo baadhi ya sumu zikiwekwa kwenye maji yasiyo na mwingilino husababisha maji kukosa hewa na maisho samaki hufa.
Wapo wanaohisi ni chemikali toka migodini. Kundi hili lisipuuzwe kwakuwa lina hoja yenye mashiko. Lakini bado kuthibitisha hili tutahitaji kujua mgodi uluopo karibu na kulipata hilo linahitaji maelezo kutoka kwa majirani na wanaozijua haswa shughuri za mgodini.