You know what man, nakubalina na maelezo yako kwa asilimia kubwa sana lakini kama alivyosema
Paulo Sergio De Souz, issue sio neno bali context! Hakuna neno baya la Kiswahili kama "mse'nge" lakini wenyewe kwa wenyewe kila wakati huwa tunaambiana "dah, we jamaa mse'nge; sikuwezi....!" yaani neno lile lile la kuchukiza na kukarahisha linageuka kuwa kivumishi depending na context na wanaombiana hivyo ni watu wa karibu! Hata huko US, black kwa black kuitana nigga isn't an offense tatizo linakuja pale White anapomuita black Nigga, especially kama sio washikaji! Humu JF ni kawaida sana mtu kuandika "Watanzania ni mazombie, mabwege, waoga n.k" lakini hatuwezi kuruhu mtu wa taifa lingine atumie maneno hayo hayo dhidi yetu-- tutamshukia! So, hata hao Wabelgiji nao wanafajamu kwamba Samatta kumuita Ulimwengu Nigga wala sio tiketi ya wao nao kumuita Samatta Nigga!