Samatta atumia 130M kununua gari yake mpya

Big up kwako Samatta
Mafanikio yako yanatokana na juhudi zako. Vijana wengi watajifunza kutoka kwako
 
Hii habari we mleta mada umeitoa wapi ........... Maana yeye niliwahi kumsikia akiongea na Salim Kikeke akisema kwamba magari huwa wanapewa na timu yao (ila inakuwa ni mali ya timu) lakini kama huwezi kuendelesha au bado hujafaulu mitihani yao ya udereva unapelekwa na dereva wa timu.
 
Ni uamuzi wake, ni pesa zake.
Lakini mimi binafsi sijavutiwa na uamuzi huo, kwa sababu sio vizuri sana kwa kijana mdogo aliyepata mafanikio makubwa ya kipesa kwa muda mfupi kisha kukimbilia kutumia pesa zake kwenye Vitu vya gharama kubwa sana kama kununua gari ya kutembelea ya kifahali. Gari ya milioni 136 la nini kwa kijana ambaye ndio kwanza anamiliki gari katika maisha yake huko Ulaya?

Wenye Hekima watanielewa vizuri.
 
Mwanaume unanunuaje gari nyekundu.. angenunua nyeusi au nyeupe kama hiyo.. sio mbaya lakini

Enzi zile hata RAV4 ziliitwa Kitchen party kwa kuwa tu Amina Chifupa ndio alikuwa miongoni mwa watu wa Mwanzo mwanzo kumiliki hapa nchini
 
ungempa hiyo €35,600 kisha ukampangia hayo masharti ''uchwara''
Watu mna majibu yapo tayari yani mtu unasubiriwa tu umwage pumba zako.you made my day.ha ha ha ha
 
neno langu sio sheria, yalikuwa ni mawazo yangu tu.. hata mwisho nimeandika sio mbaya.. peace
Ndio ukome kuleta mawazo mavimavi!nyie hakunaga kupongeza ni mwendo wa kupinga tu as long as hicho kilichotokea kinauhusiano na mtanzania au tanzania!
 
Ndio ukome kuleta mawazo mavimavi!nyie hakunaga kupongeza ni mwendo wa kupinga tu as long as hicho kilichotokea kinauhusiano na mtanzania au tanzania!
hahah huwezi kuniprovoke mkuu, mimi sio mtu wa mchezomchezo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…