Samatta atumia 130M kununua gari yake mpya

Samatta atumia 130M kununua gari yake mpya

chinchilla coat

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2016
Posts
5,107
Reaction score
10,969
xSamatta.jpg.pagespeed.ic.rTpXCEDMup.jpg


Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta ametumia kiasi cha milioni 130 kununua gari yake ya kwanza nchini Ubelgiji.
Gari hilo alilonunua mchezaji huyo ni Benz Cla220 Cdi AMG Sport 2016 ambayo gharama yake inadaiwa kuwa ni €46,680.

Samatta amechukua uamuzi huo baada ya kufanikiwa kupata leseni inayomruhusu kuendesha gari nchini humo baada ya kunyimwa miezi kadhaa iliyopita.

Inadaiwa kuwa mchezaji huyo analipwa kiasi cha €35,600 kutokana na mkataba wake wa kuichezea timu ya Genk ambao utamalizika mwaka 2020.

Kwa sasa Samatta ameonekana kuwa miongoni mwa wachezaji wa kutegemewa kwenye timu ya KRC Genk ambayo inashiriki kwenye michuano ya Europa League japo amekuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili akiuguza majeraha.
 
Nani alikwambia mwanaume haruhusiwi kuendesha gari nyekundu? Kwa taratibu za wapi kuanzia lini?
neno langu sio sheria, yalikuwa ni mawazo yangu tu.. hata mwisho nimeandika sio mbaya.. peace
 
spacial kwa chick hiyo likiwa kwenye parking sehemu yoyote ndio la kwanza kuonekana...pia special kwa kuikumbuka timu yake iliyomfikisha hapo
pengine, hata wewe neno lako sio sheria pia
 
Back
Top Bottom