Kwanza asante kwa:-
1. Kutilia mashaka UANAUME Wangu. (Japokua nimeshindwa kuelewa unawezaje kujua jinsia za members wa humu ndani)
2. Kutuita wapumbavu na huyo "mp.umbavu mwenzangu" (nadhani ulimlenga nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania).
Pili;-
Unaweza ukawa unamaanisha nini labda unavyosema mtu kapata hela na THE FIRST THING Kununua ni gari ya 130M ? Unataka kutuambia hata saa ya mkononi, kijiko, glasi, sturi, kiwanja, nyumba n.k hana ?
Hata ikiwa hivyo vyote hana, U nani wewe hata umpangie nini aanze kununua nini afuate ?
Unajua hata angenunulia bia hela zake zote yuko sahihi maana hela ni mali yake na anapata kwa njia halali!
Sijui huko mtaani kwenu unaishije na majirani kwa hili gubu, mtu asinunue bodaboda, smartphone, kitenge, suruali mpya, mafuta ya kupakaa etc halafu ukajua utaongea wiki nzima na hizo critics zako.
Nitoe RAI tu kwa MBWANA ALLI SAMATTA POPPAT, kaka saizi nunua BOMBARDIER kabisa umnyooshe huyu.
LoveYou