Samatta azidi kutisha huko Belgium

born again pagan

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2014
Posts
2,336
Reaction score
1,491
Mshambualiaji hatari wa Taifa Stars na mchezaji wa zamani wa Simba na TP Mazembe ambaye kwa sasa anakipiga kwenye club ya KRC Genk ya huko Belgium inayoshiriki ligi kuu ya huko ijulikanayo kama Pro league.

Jana 21 august Genk ilicheza mechi yake ya 4 tangu msimu huu uanze na walicheza wakiwa ugenini dhidi ya Lokeren.

Kama kawaida Samatta alikuwepo kwenye starting XI akimuweka bench nguli kutoka Greece Nikos Karelis. Kwenye mchezo huo ulioanza majira ya saa 1 ucku EAT Genk walishinda 3-0.

Samatta alitupia mawili dk 34 na dk 38 hadi HT Genk wanaongoza. Second half dk 59 mchezaji T. Buffel aliongeza bao la tatu na kuitimisha ushindi mnono wa Genk.

Kwa matokeo hayo sasa,Genk imefikisha points 7 na kushika nafasi ya 4. na Samatta amefikisha magoli 3 in 4 matches.

Bravo Samatta.


Updates....................!!!!!!!

Mechi za Europa league au Uefa ndogo jana tarehe 25 August 2016 ziliendelea kama kawaida kutafuta kufuzu kwenye makundi.

Kijana wetu Samatta na chama lake la Genk walikuwa dimbani kupepetana na Locamotiva Zagreb ya Croatia.

Ikumbukwe mchezo wa kwanza hizi timu zilitoka sare ya 2-2.
Jana Genk ilishinda bao 2-0 magoli yakifungwa na home boy Samatta dk 2 tu ya mchezo na bao la pili lilifungwa na Mjamaica Bailey dk 50.

Kwa ushindi huo sasa,Genk imefuzu Europa league group stage ambayo yatapangwa Leo.

Swali dadisi.
"Je Samatta kuivaa united"

Stay tuned.
 
Kila la kheri kwake, Pale Belgium ndio njia panda ya kuingia ligi zote kubwa duniani
 

Mkuu umetoa thread nzuri kwa ajili ya nchi yetu uzalendo kwanza ila goli la tatu ameshinda dogo shujaa wa jamaica leon bailey
 
Samatta atawafunga sana Wabelgiji.

Unajua alifika kipindi kigumu sana wakati timu yake ikiwa na mechi ngumu tupu, yaani zile mechi cha mwishoni mwa ligi, kisha Nane Bora. Sasa hivi ameianza ligi tangu mwanzo ana nafasi kubwa ya kufunga zaidi
 
Hongera sana Ali Samatta! Ila thread zimezidi mno kumpamba, kiasi kwamba wadau wanashindwa wachangie vipi, mfano; kuna thread nyingine imeanzishwa ya magoli to... sasa kwanini hayo magoli yasiambatanishwe na huu mjadala
 
Naona kwa sasa nchi yetu imeanza kutake off katika kila idara, tukiacha siasa tutaweza kuliona hilo na sifa zitakuwa juu ya watanzania kwa ujumla. Umoja ni maendeleo na maendeleo siyo siasa, maendeleo ni mipango chini ya uzalendo na kujituma sote kwa pamoja.
 
Jamani hivi yule mchezaji wa azam alienda Spain ameishia wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…