Samatta kuonekana UEFA au Ligi Kuu ya England. BIG up jembe la Tanzania

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,104
Reaction score
6,827
Je, Samatta kucheza Klabu Bingwa Ulaya na Genk ama kutimkia England msimu ujao?

Samatta na tuzo

Samatta amefunga zaidi ya magoli 30 msimu huu akaiwa na klabu ya Genk.

Mshambuliaji nyota wa mabingwa wa ligi ya Ubelgiji klabu ya Genk na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta huenda akatua Ligi Kuu ya England (Primia) msimu ujao.

Samatta, maarufu kama Samagoal, amedokeza kuwa kuna vilabu sita vya Ligi ya Primia ambavyo vinapigana vikumbo kumsajili.

"Kwa sasa sipo katika nafasi nzuri ya kuelezea ni klabu gani lakini pia kuna klabu nyingine mbili kutoka Hispania ambazo zimekuwa zikiisaka saini yangu. Hata hivyo, mimi ndoto zangu ni kucheza katika Ligi Kuu ya England," Samatta ameliambia gazeti la Mwananchi.

Hii si mara ya kwanza kwa Samatta kuhusishwa na uhamisho wa kwenda Ligi ya Primia, lakini inaonekana kuwa safari hii mambo yameiva.

"Ndiyo, nitaondoka mwishoni mwa msimu huu...(klabu ya England) moja inanifukuzia sana na imekuwa ikipiga simu kwa wakala wangu kila siku," amesema Samatta.
https://ichef.bbci.co.uk/news/485/cpsprodpb/3AED/production/_107058051_gettyimages-1148241427.jpg[/IMG

Samatta amechezea klabu ya Genk kwa misimu mitatu sasa.

Katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari mwaka huu, klabu ya Cardiff ilituma ofa ya Pauni milioni 13 kumng'oa Genk, lakini uhamisho huo ukakwama.
Klabu ya hata hivyo Cardiff imeshuka daraja.

Ukiachana na Cardiff, vyombo vya habari vya Uingereza mwaka jana viliripoti klabu nyingine tatu za nchini humo ambazo zilikuwa zikihusishwa na kutaka huduma ya ushambuliaji kutoka kwa Samatta.

Klabu hizo ni Everton, WestHam na Burnley.
[SIZE=6][B]Kipenzi cha mashabiki Genk[/B][/SIZE]
Samatta ameendelea kuwa kipenzi cha mashabiki wa Genk msimu huu baada ya kuongoza safu ya ushambulizi wa timu hiyo na kunyakuwa ubingwa wa ligi hiyo baada ya kuukosa kwa miaka nane.

Streka huyo mwenye miaka 26, ameifungia Genk magoli 23 na kumaliza kama mshambuliaji bora wa ligi. Pia ameifunga magoli 9 kwenye michuano ya ligi ya Europa.

Jina la Samatta limekuwa likiimbwa na mashabiki wa Genk, na wamekuwa wakimuomba mshambuliaji huyo kusalia klabuni hapo kucheza ligi ya Mabingwa Ulaya.

Samatta ameiambia Mwananchi kuwa moyo wake upo England japo kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi ya Mabingwa ni kitu cha kutamanisha pia.
[IMG alt="Samatta"]https://ichef.bbci.co.uk/news/485/cpsprodpb/890D/production/_107058053_2b325706-2cab-4e3c-ae93-6f9da88c9837.jpg

Samatta alipohamia KRC Genk 2016
Hata akihamia England, bado atakuwa ameweka rekodi ya kuwa mtanzania wa kwanza kufanya hivyo. Pia amekuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi ya Europa.

"Hawa jamaa (Genk) hawajacheza Ligi ya Mabingwa tangu mwaka 2011 enzi za akina (Kevin) De Bruyne, najua wanataka nicheze msimu ujao lakini Ligi Kuu ya England ina heshima yake...ni ligi ambayo tayari imepiga hatua kubwa sana kulinganisha na Ligi Kuu ya Ubelgiji.

Ni ligi ambayo inapendwa na watu wengi duniani, Ligi inayoonekana sehemu kubwa duniani. Yaani kwa vitu vingi iko mbali."
 
Samatta ni bora abaki Genk kuliko kwenda EFL ama EPL akacheze timu itakayoshuka daraja.

Samatta hana kiwango cha kupata namba kwa uhakika EPL ligi ile ni ya nguvu sana na maarifa, Jupiter league ni mdebwedo sana sibezi mafanikio yake ila ndio ukweli mara elfu 10 abaki Genk akacheze UEFA kuliko kwenda Swansea au stoke city kwa sasa asubiri awe mtambo mkubwa.

Alicheza EUROPA na vitimu vya ajabu ajabu akafunga sanaa alipokutana na Fernebahce ndipo akauona mpira wa ulaya ulivyo mara slavia Prague HAHAHAA Samatta ndugu yangu komaa na Genk
 
Shukran za Pekee ziende kwa Rais wa Jamhuri na Waziri wa Michezo kwa sera madhubuti na rafiki zinazowezesha mambo kama yenye kuwezekana wakati wa uongozi wao ikiwa ni pamoja na Timu yetu ya Taifa kufikia fainal za Mataifa huru ya AFRICA baada ya Miaka 40 (1979-2019)
 
wanyakyusa mmekalia majungu
 
Ana Mashabiki Wengi Nchini, Ila Kwa Kujenga Msikiti Ndani Ya Jumba Lake Ni Udini Mtupu, Bora Ajenge Jumba Jingine Na Ndani Yake Aweke Kanisa Itapendeza Sana Kwa Mashabiki Wake Wasio Waislam
Angejenga shule au hata clinic ingependeza zaidi.
 
Samatta ni bora abaki Genk kuliko kwenda EFL ama EPL akacheze timu itakayoshuka daraja.

Samatta hana kiwango cha kupata namba kwa uhakika EPL ligi ile ni ya nguvu sana na maarifa, Jupiter league ni mdebwedo sana sibezi mafanikio yake ila ndio ukweli mara elfu 10 abaki Genk akacheze UEFA kuliko kwenda Swansea au stoke city kwa sasa asubiri awe mtambo mkubwa.

Alicheza EUROPA na vitimu vya ajabu ajabu akafunga sanaa alipokutana na Fernebahce ndipo akauona mpira wa ulaya ulivyo mara slavia Prague HAHAHAA Samatta ndugu yangu komaa na Genk
Alivyowatungua Besiktas goli mbili hilo haukuliona?au Besiktas ni timu mdebwedo kuliko Fernebahce?

Pia hiyo mechi na Fernebahce ilichezwa lini na wapi?
 
Shukran za Pekee ziende kwa Rais wa Jamhuri na Waziri wa Michezo kwa sera madhubuti na rafiki zinazowezesha mambo kama yenye kuwezekana wakati wa uongozi wao ikiwa ni pamoja na Timu yetu ya Taifa kufikia fainal za Mataifa huru ya AFRICA baada ya Miaka 40 (1979-2019)
Wamefanya nini hao uliowataja kwa Samatha?
Taifa Star wenyewe washukuru Uganda hawakuwa na cha kupoteza
 
Samatta ni bora abaki Genk kuliko kwenda EFL ama EPL akacheze timu itakayoshuka daraja.
Samatta hana kiwango cha kupata namba kwa uhakika EPL ligi ile ni ya nguvu sana na maarifa, Jupiter league ni mdebwedo sana sibezi mafanikio yake ila ndio ukweli mara elfu 10 abaki Genk akacheze UEFA kuliko kwenda Swansea au stoke city kwa sasa asubiri awe mtambo mkubwa.
Alicheza EUROPA na vitimu vya ajabu ajabu akafunga sanaa alipokutana na Fernebahce ndipo akauona mpira wa ulaya ulivyo mara slavia Prague HAHAHAA Samatta ndugu yangu komaa na Genk

Hahaha naona umetema cheche nondo za ukweli mtupu. Ligi ya EPL mwenywe sidhani kama ataiweza kama shevchenko aliishindwa 🤣🤣. Ila sijambeza natambua uwezo wake ni mkubwa sana watanzania tunajivunia kua na yeye.
 
Shukran za Pekee ziende kwa Rais wa Jamhuri na Waziri wa Michezo kwa sera madhubuti na rafiki zinazowezesha mambo kama yenye kuwezekana wakati wa uongozi wao ikiwa ni pamoja na Timu yetu ya Taifa kufikia fainal za Mataifa huru ya AFRICA baada ya Miaka 40 (1979-2019)

Siasa na mpira haviendani acha uzwazwa wewe popoyo. Hakuna sera wala juhudi yeyote aliyofanya huyo unayemshukuru. AFCON tumebahatisha kwenda na pia ni wachezaji tu wenyewe wamekua na muamko kipindi hichi kutokana na mahudhurio ya washabiki kujaza taifa na mafanikio ya kina Samatta na Simba kimataifa la siivyo hakuna mchango wa serikali kabisa maana sera zetu ni mbovu sana na utekelezaji ni sifuri.
 
Hizo bahati na hamasa tangu 1979 zilikuwa wapi?

Kongole Dr Magufuli
 
Back
Top Bottom