Samatta kwenda Uturuki tumpe Hongera au Pole?

Samatta kwenda Uturuki tumpe Hongera au Pole?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kuna wanaosema ni bora aende Uturuki akapate nafasi ya kucheza na kuna wanaosema kutokana na umri wake kiwango chake kimeshuka na kinakwenda kushuka zaidi huko Uturuki bora angebaki tu EPL.

Ukweli ni upi?

Kwani ligi ya Uturuki na ile ya Ubelgiji alikokuwa ni bora ipi?
 
Angebakije EPL wakati ASTON VILLA hawamtaki na hakuna team nyingine iliyoonesha interest?

Huyu kiwango kimeshuka na motivation kwisha kabisa. Kocha wake alisema hata mazoezini tu haonyeshi juhudi. Inabidi akajipange upya huko aendapo.
 
Angebakije EPL wakati ASTON VILLA hawamtaki na hakuna team nyingine iliyoonyesha interest?

Huyu kiwango kimeshuka na motivation kwisha kabisa. Kocha wake alisema hata mazoezini tu haonyeshi juhudi. Inabidi akajipange ipya huko aendapo
Kuna watu hawapendi kusikia Samatta anakosolewa kwa lolote. Samatta alikuwa anasoma comments za mitandaoni kuhusu yeye zaidi kuliko kujikita kwenye lile lililompeleka AV.
 
Akacheze uturuki kuliko kukaa benchi Villa. siku nyingine washaurini watoto wenu wasidanganye umri maana kila kitu wataona wanaonewa, akili inataka mwili unakataa.
 
Samata yupo Aston villa. Shafii Dauda asikupotoshe.
 
Kubaki Uingereza ni mpaka wenyewe wakutake, kama hawakutaki utafanyaje? Ligi ya Uturuki ni ya 11 kwa ubora duniani, so ni bora kaenda huko
 
Kuna watu hawapendi kusikia Samatta anakosolewa kwa lolote. Samatta alikuwa anasoma comments za mitandaoni kuhusu yeye zaidi kuliko kujikita kwenye lile lililompeleka AV
Samatta sio mjinga wa kiasi hiki, ni mtu anayejielewa na ni mtu anayejituma sana kwa mazoezi, ni kwamba AV hawamtaki haina maana kuwa hafai kwingine
 
Behaviourist,

Hakuna mtu anaehangaika na kuvuja jasho kama Samatta akabaki kuwa fukara hata kama anauza chuma chakavu au kupara samaki. kuwa tajiri sio lazima kucheza mpira AV bali fanyakazi yoyote kwa juhudi na maarifa na kwa moyo wako wote. Ingemshangaza kila mtu kama samatta akiwa fukara hata baada ya kuwekeza akili na nguvu nyingi kwenye jambo lake. Wewe ndio usiyependa samatta aguswe.
 
akacheze uturuki kuliko kukaa benchi villa. siku nyingine washaurini watoto wenu wasidanganye umri maana kila kitu wataona wanaonewa, akili inataka mwili unakataa
Kwa manufaa ya wananchi wake kimataifa ni vizuri ni vizuri mifumo yote kijamii, kisiasa, kiuchumi na taarifa ya kila nchi ikawa ya wazi na kuaminika kitaifa, kikanda na kimataifa pia.
 
Samatta sio mjinga wa kiasi hiki,ni mtu anayejielewa na ni mtu anayejituma sana kwa mazoezi,ni kwamba AV hawamtaki haina maana kuwa hafai kwingine
Kila mtu ana ndoto ya kucheza EPL, ina maana timu zooooote za EPL hazimtaki, amewafanya nini au hakufanya nini EPL?
 
Watanzania tunachekesha sana, nadhani umasikini umetuathiri sana kisaikolojia, mtanzania anaweza kuchambua maisha ya mtu kiasi kwamba hata yule mhusika akashangaa sana.
Ukiwa maarufu huwezi kuyakwepa haya. Inawezekana wewe ni mwanachama hai wa CCM
 
Back
Top Bottom