Samatta Vs Msuva Timu Ya Taifa!

Samatta Vs Msuva Timu Ya Taifa!

Huyu sio samata ni Molinga aliyechangamka
Hapa kunawatu wanashindwa kuelewa hatumlaumu samatta kwakua tumefungwa, Hata tungesginda Ila bado tusingeridhishwa na kiwango anachoonesha samatta katika timu ya taifa. Wote tunajua kua huu sio uchezaji wa samatta Bali anajilinda asipate majeruhi. Hali hii inapelekea atoe msaada kidogo Sana katika timu.

Tutaendelea kumlaumu samatta Kama akiendelea kucheza namna hii Kama anaogopa majeruhi Basi ahakikishe hapotezi mipira ambayo wachezaji wenzake wanaangaika kuicover yeye anapoteza kirahisi anawashusha morali wachezaji wenzake na pia anapelekea kutokea makosa mengi mpaka kupoteza mchezo.

Ni muda sahihi Sasa kutomtegemea samatta katika timu ya taifa Bali tuwape nafasi wachezaji wengine waoneshe ushindani katika namba ya samatta anatuangusha Sana.
 
Ukienda Mbagala watu wanashangaa Mbwana kawezaje kucheza Ulaya wakati fundi kaka yake anamaliza soka Bongo...uchawi upo
 
Kocha nalo senge tu, we mmefika dk ya 60 unashindwa kujaza viungo na kuvuruga mipango tu ya Libya?? Msuva naye wakati mwingine ingia Kwnye 18, siyo kila muda unapiga cross tu.

Na tutolewe tu watu wapumzike!!
 
we umesimamia kucha hapa ila siku akifanya vizuri utakuja tena kusifia ndo wabongo mlivyo baya la siku1 unasahau mazuri yote bila kujua kila kitu kina wakati wake
Lini kafanya vizuri toka yuko mazembe ni hivi hivi tu
Hata huyu farid hamna kitu boravwaitwe madogo wa chan waongezewe msuva basi hawa wa ulaya mizunguo tu
 
Lini kafanya vizuri toka yuko mazembe ni hivi hivi tu
Hata huyu farid hamna kitu boravwaitwe madogo wa chan waongezewe msuva basi hawa wa ulaya mizunguo tu
Mechi nyingi tu ameibeba Taifa stars kwani mpira umeanza lini kuangalia
 
Samatta alishayumba tangu game ya Dar.

Imeniuma sana, ile game ilikuwa ya kuchukua point tatu kabisa japo hata refa alitunyonga.
 
Baada ya kumfuatilia Sana Samatta akiwa na Timu Ya Taifa nimeamua Kuandika Huu uzii na Kusema kuwa Simon MSUVA ni Bora Zaidiiii Kuliko Samatta Katika Timu ya Taifaa, Bado Samatta hajaonesha kiwango chochote timu Ya Taifa kama Afanyavyo Msuva, Samatta Amekuwa Akicheza kwa Tahadhari mnoooo kuliko mchezaji yoyote na amekuwa anapoteza mipira kirahisi sanaaa kwa kuhofia kuumiaa! nadhani Anajitahadhari kwa sababu Anaogopa Asije akaumia timu ya Taifa Na kushindwa kucheza ulaya! Hii inafanya ashindwe hata kujitumaa kama wachezaji wengine! Angalia Msuva Anavyocheza akiwa na Timu ya Taifa,angalia Striking force ya Msuva Na Wachezaji wengine Ni tofauti kabisa na Timu na Samatta! Yule Samatta Wa Genk sio huyu wa Timu Ya Taifa

Ni wakati sasa Wa Timu ya Taifa Kuacha Kumtegemea Samatta kama mchezaji wao anaeweza kunadiri matokeo muda wowote hapana! Ni wakati sasa Wa Timu Ya Taifa Kukomaa na Local Players Wetu pamoja na Msuvaa, ni wakati sasa wa Makocha kuanza kumfanyia Sub Samatta na Kuacha vijana wengine waoneshe Uwezo Wao!

Samatta anawadanganya hata Makocha na kusabisha makocha waogope hata kumfanyia Sub au kumuacha Kumuita Wakihofia Kusemwa na Majungu ya Watanzania ila Kiuhalisia Samatta Timu Ya Taifa Hana Msaada kama Akiwa Genk! Angalia Msuva Anavyo tafuta magoli na Ku creat chances nyingi sana tofauti sana Na Samatta

Kwangu Mimi Sijaona Kipya cha Samatta Akiwa Na Timu ya Taifa,Kwangu Mimi Msuva Ni Bora Kuliko Samatta katika Ngazi ya Timu ya Taifa,Msuva Ni wakati sasa Wakwenda Ulaya

Samatta Wa Genk sio Wa Taifa Stars
Bora wacheze akina Chilunda na Nado dak 90 lakini sio Samatta,natambua uwezo wake lakini ni ukweli ulio wazi kwamba hivi karibuni akiwa timu ya taifa amekuwa hajitumi kabisa.

Naunga mkono hoja.
 
Mbona walifanya vizuri dhidi ya Sudan bila kina Samata na Msuva ?
Alikua bora ktk ufungaji ligi ya kongo drc na mazembe,mpaka kugombea mchezaji bora afrika
Amekua mfungaji bora ktk ligi ya ubelgiji mpaka kufikia kuibeba genk kuteaa ubingwa na kuipeleka Uefa
Amefanikiwa kuwa mtz wa kwanza kucheza Uefa na kuzifumania nyavu za mabingwa wa ulaya home and away-anfield-licha ya kukabwa na mabeki wazoefu akiwemo beki bora ulaya..!....vipi leo awe mbovu?
Tatizo halipo kwa samata jiulize samata anacheza na akina nani uwanjani?
Kiukweli wachezaji wetu ukiondoa labda msuva wana viwango duni mno!wengi uzoefu hawana,ball control,speed &accuracy vipo chini mno...hilo ndio tatizo..Sama goal wanamuimba pale genk acha kabisa!
 
Mechi ya jana ukiachana na maamuzi mabovu kama tungekuwa makini tungeshinga. Wachezaji wetu wanakosa umakini, makosa wanayofanya ni mengi mno na ndio yanatugharimu. sasa mtu unafanya tackling ndani ya 18 unategemea nini, kuna beki mmoja alicheza faulo ndani ya 18 na refa akapeta, wachezaji wetu waongeze umakini hata kama viwango ni vidogo.
 
Samata kule genk anawika sababu kuna mastaa wanambeba na kumpa sapoti kubwa, samata sio ball dribbler kama msuva Bali ni mmaliziaji
 
Mbwwna Samatta ameanza kupata changamoto kubwa pale Genk kwani ujio wa Koch's mpya. H. Wolf toka Ujerumani umeanza kumfanya awe chaguo LA pili (kuanzia bench) katika ushambuliaji. Leo ni mechi ya pili namwona Mbwana Samatta akianzia benchi dhidi chaguo LA kwanza kwa sasa .P. Unuachu toka Nigeria.
 
Mbwwna Samatta ameanza kupata changamoto kubwa pale Genk kwani ujio wa Koch's mpya. H. Wolf toka Ujerumani umeanza kumfanya awe chaguo LA pili (kuanzia bench) katika ushambuliaji. Leo ni mechi ya pili namwona Mbwana Samatta akianzia benchi dhidi LA kwanza kwa sasa .P. Unuachu toka Nigeria.

Yaaa ila Genk msimu huu hamna kitu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom