~^^~ Sambusa ni tamu bwana! ~^^~

~^^~ Sambusa ni tamu bwana! ~^^~



Sambusa ni tamu bwana,
Nyingine hakuna tena,
Wa kijiji ninanena,
Vingine sijaviona! - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Ukishaonja sambusa,
Vitumbua utasusa
Na utatumia mapesa,
Uje upate sambusa! - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Na zile zenye mafuta
Ulimini zinanata,
Na ladha ukishapata
Waweza tangaza vita - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Zipo zenye nyamanyama
Zaliwa Kijitonyama
Hata ukenda Dodoma
Sambusa hutojinyima - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Zipo zile zenye mboga
Zilochumwa kama boga
Wale wasio waoga
Wazila hata Msoga! - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Zipo zenye vitunguu
Zilotiwa karafuu
Ukila mluzi huu
Waimba "mikono juu" - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Na sambusa za Kihindi,
Utazikuta Malindi
Hata Mtwara na Lindi
Zinapikwa na mafundi! - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Uonje 'zopikwa Tanga
Ngonjera utazitunga
Ukipata za Iringa
Na baridi la Mafinga - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Beti zangu nazifunga
Tungo nimeshazipanga,
Sambusa sitojivunga
Nayeya ninapuyanga
SAMBUSA NI TAMU BWANA, HASA ZISIZOFANANA!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)

funza ninasimama, sambusa kuzitizama
macho yanipima, kwa kudunda kwa mtima
mate yaniwama, mdomoni yamekwama
Napata hamu nasema, sambusa nikitizama
 
Nyingine ni za kichina
Zilizotuna kwa sana
Na zipo za Amerikana
Azipikazo Shaquana!
Sambusa ni tamu bwana, hasa zisizonana!
 
Nyingine ni za kichina
Zilizotuna kwa sana
Na zipo za Amerikana
Azipikazo Shaquana!
Sambusa ni tamu bwana, hasa zisizonana!

Mimi napenda pie
Ile pootang pie
Usidhani nazumgumzia papai
Hizo sambusa zako hazioni ndani
Utamu wake kama sukari
Mdomo wangu umebaki wazi

Ijaribu siku moja
Hakika itakunogea
Ikikudatisha
Usije kudhani ni kashata
Ukaja kuichanganya na ufuta
 
Duh! Mkjj nimekubali wee ni Malenga kinoma.
WoS nawe unatisha!
-----
Tuache utani watani
Sambusa ni tamu jamani
Nani asiyeitamani?
Si haramu asilani
Nzi kufia kidondani

Kitumbua tusisahau
Vipi laini za simu?
Voda na Tigo wadau?
Ukipewa huishi hamu
Utataka kula kila siku
 
Mie pia naafiki, kwamba sambusa ni tamu hazishindi bata mchafu kama niliyemla nyumbani kwa binamu ambaye alikolea pilipili, limau na chumvi bla kuzidi hata kidogo hahahahahah
 
Back
Top Bottom