Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Leo huko DODOMA wametangaza rasmi wagombea wa CCM wa nafasi ya rais wa JMT na rais wa Zanzibar.
Kama mnavyojua kwenye siasa hakuna kitu cha bahati mbaya, ni dhahiri huo mpango wa kumpitisha Samia na Hussein Mwinyi kuwa wagombea kwa Kuwashtukiza wanachama ulisukwa mapema. Kwa hiyo hata kikao hiki cha kwenda kumtafuta makamu mwenyekiti kilikuwa zuga tu, lengo lilikuwa ni kumteua rasmi Samia kuwa mgombea wa Urais.
Hii maana yake nini, maana yake Samia kapita bila kufuata mchakato wa kawaida wa chama wa kuchukua fomu kutafuta wadhamini kutoka mikoa mbalimbali nchini. Na Hussein Mwinyi naye kakwepa mchakato wa kumtafuta Mgombea Urais huko Zanzibar. Ule Msemo wa Rais wa Zanzibar anatokea DODOMA Tanganyika umedhihirika leo.
Hiki alichokifanya Samia na kaka yake Hussein Mwinyi ni Kutafuta mteremko wa kisiasa na Unajenga Precedence moja mbaya sana. Sasa hivi wana CCM wajue tu kuwa in the future, hakuna Rais atakayetokana na chama hicho atakayejali hatua za vikao kadha wa kadha, yeye atakuwa anacheza na mkutano mkuu tu , mkutano ukishasema ndiyoooooo, hakuna cha mkutano wa halmashauri kuu wala kamati kuu utakaokuwa na sauti juu ya maamuzi mbalimbali mazito.
Staili hii hii Samia anaweza kuitumia kuilazimisha CCM iridhie ubadilishaji wa katiba kuondoa muhula wa vipindi vya uongozi au kuongeza muda.
Kwa kweli hii staili ya Mbereko, ya kupitisha watu bila kupingwa, ya kutafuta mbereko kwa kukwepa ushindani wa kisiasa ndani ya chama, CCM imeulea yenyewe na sasa madhara yanawarudia wao. Hakuna tena kufuata due process ya kupata wagombea, ni kuwashtukiza wajumbe tu walioshiba ubwabwa, na kulipiwa guest house za kufikia ili watoe sauti za ndiyooooo.
Hii ni disaster.
Leo Samia amekoleza safari ya CCM kujifia, kimegeuka chama cha maigizo, hakuna brainy aspects ya kila move chama hiki kinafanya kwa sasa. Kimegeuka kama chama cha sherehe ya wachoma nyama kula mapande ya minofu ya nchi bila kujali mustakbali wa vizazi vijavyo.
Yetu macho, lakini kwa sasa hakuna chama hapo ni genge la watafuna nchi huku likiwarushia wajumbe makombo ya posho kipindi cha vikao kama hivi vilivyotawaliwa na upambe, uchawa, mob psychology na group thinking.