The-unknown
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 1,228
- 1,447
Yani hajiamini hata kidogo,na mchakato wa kawaida ungetumika ndo kabisaa angewekwa mbali,Kwa namna yoyote Rais Samia anaweza kusimamishwa kama mgombea urais wa CCM na kushinda uchaguzi ujao. Huenda Rais Samia hajihamini au hana uhakika kama atatetea kiti cha urais ndio maana anaharakisha mchakato tena kwa kushtukiza. Kama imepangwa kuwa ndivyo itakavyokuwa. Bado ni parefu kufika October.
Lah..kumbe..?Wapi wewe kakojoe kanye ulale...
Utakua wa mfano na wa pekeeeSubirini uchaguzi wenu J4.
Hawapo seriousNi maajabu CCM kutangaza mgombea kabla hata haijatangaza kutoa fomu ya kuomba kugombea. Hiki chama kina magumashi mengi.
Leo Jakaya kacheza kama pele π₯π₯Ilikuwa tusubiri mpaka mwezi wa tano, lakini yupo mjumbe wa Mwanza ambaye alitia mashaka kuendana na vifungu vya katiba ya chama, ( Kisaikolojia akimaanisha kuna watu waliokuwa wakijiandaa kugombea kwa siri waje wajitokeze kwa njia ya mlipuko, Akili ikawacheza baada ya kushauriana na mzee wetu jakaya, ikaonekana ni bora ukurasa ufungwe mapema sana ikibidi leo leo) hivyo wale wote waliokuwa na vikao vyao vya siri imekula kwao, huku mambo ya form, au form ni moja tu, nampongeza bwana Jakaya, zakusikia changanya na zako, Samia mitano tena, hao jamaa wangekuja jitokezeni kwa ghafla kama Lisu alivyomfanyia mbowe, alamsiki
Umenena neno. Uswahili hapo ndio umefanyika. Umekumbusha katiba na taratibu. Mgombea lazima apite kupata sahihi za wanachama kuunga mkono uamuzi wake kutaka kugombea. Huu uhuni unatoka wapi? Ukimuona mtu anajiita 'Dr' Nchimbi ujue kwake ni mambo ya kihuni tu. Kwa ufupi uteuzi huo ni non and void maana ni kinyume na katiba na taratibu za ccm. Mpango mzima wa kushtukiza ni uhuni mtupu.Leo huko DODOMA wametangaza rasmi wagombea wa CCM wa nafasi ya rais wa JMT na rais wa Zanzibar.
Kama mnavyojua kwenye siasa hakuna kitu cha bahati mbaya, ni dhahiri huo mpango wa kumpitisha Samia na Hussein Mwinyi kuwa wagombea kwa Kuwashtukiza wanachama ulisukwa mapema. Kwa hiyo hata kikao hiki cha kwenda kumtafuta makamu mwenyekiti kilikuwa zuga tu, lengo lilikuwa ni kumteua rasmi Samia kuwa mgombea wa Urais.
Hii maana yake nini, maana yake Samia kapita bila kufuata mchakato wa kawaida wa chama wa kuchukua fomu kutafuta wadhamini kutoka mikoa mbalimbali nchini. Na Hussein Mwinyi naye kakwepa mchakato wa kumtafuta Mgombea Urais huko Zanzibar. Ule Msemo wa Rais wa Zanzibar anatokea DODOMA Tanganyika umedhihirika leo.
Hiki alichokifanya Samia na kaka yake Hussein Mwinyi ni Kutafuta mteremko wa kisiasa na Unajenga Precedence moja mbaya sana. Sasa hivi wana CCM wajue tu kuwa in the future, hakuna Rais atakayetokana na chama hicho atakayejali hatua za vikao kadha wa kadha, yeye atakuwa anacheza na mkutano mkuu tu , mkutano ukishasema ndiyoooooo, hakuna cha mkutano wa halmashauri kuu wala kamati kuu utakaokuwa na sauti juu ya maamuzi mbalimbali mazito.
Staili hii hii Samia anaweza kuitumia kuilazimisha CCM iridhie ubadilishaji wa katiba kuondoa muhula wa vipindi vya uongozi au kuongeza muda.
Kwa kweli hii staili ya Mbereko, ya kupitisha watu bila kupingwa, ya kutafuta mbereko kwa kukwepa ushindani wa kisiasa ndani ya chama, CCM imeulea yenyewe na sasa madhara yanawarudia wao. Hakuna tena kufuata due process ya kupata wagombea, ni kuwashtukiza wajumbe tu walioshiba ubwabwa, na kulipiwa guest house za kufikia ili watoe sauti za ndiyooooo.
Hii ni disaster.
Leo Samia amekoleza safari ya CCM kujifia, kimegeuka chama cha maigizo, hakuna brainy aspects ya kila move chama hiki kinafanya kwa sasa. Kimegeuka kama chama cha sherehe ya wachoma nyama kula mapande ya minofu ya nchi bila kujali mustakbali wa vizazi vijavyo.
Yetu macho, lakini kwa sasa hakuna chama hapo ni genge la watafuna nchi huku likiwarushia wajumbe makombo ya posho kipindi cha vikao kama hivi vilivyotawaliwa na upambe, uchawa, mob psychology na group thinking.
Umenena neno. Uswahili hapo ndio umefanyika. Umekumbusha katiba na taratibu. Mgombea lazima apite kupata sahihi za wanachama kuunga mkono uamuzi wake kutaka kugombea. Huu uhuni unatoka wapi? Ukimuona mtu anajiita 'Dr' Nchimbi ujue kwake ni mambo ya kihuni tu. Kwa ufupi uteuzi huo ni non and void maana ni kinyume na katiba na taratibu za ccm. Mpango mzima wa kushtukiza ni uhuni mtupu.
Iiih, kwa kweli , aiseeeh !K
Kwa muktadha huo je Wapinzani wao watakuwa wamefurahi au watakuwa wamechukia CCM kujifia yenyewe ??!β
π π
Acha inyeshe paonekane panapovuja !
Na ni bora uongezwe muda wa Rais kukaa madarakani maana itapunguza mzigo wa kugharamia Uchaguzi kila baada ya miaka mitano !
Huko kucheza kwake Pele kumeisaidiaje CCM kuimprove?Leo Jakaya kacheza kama pele π₯π₯
Bado..ana Mitanoyule wa zanzibar si tayari amekaa madarakani miaka 10 au bdo?
Wajanja wangegeuza meza dadek, alhamdulilah kila kitu kimegunduliwa na kimewekwa sawa.Leo Jakaya kacheza kama pele π₯π₯
Sababu ya uongo hiyo, hakuna wa kushindana na raisi aliye madarakani. Hizo zingine ni hofu tuWajanja wangegeuza meza dadek, alhamdulilah kila kitu kimegunduliwa na kimewekwa sawa.
CHama kama chamaInasikitisha, CCM yangu ya sasa inatuweka uchi kwenye democracy
Kwanini lakini?!!
Si ninyi mliosema unatumia dola kubaki madarakani?Yani hajiamini hata kidogo,na mchakato wa kawaida ungetumika ndo kabisaa angewekwa mbali,
Pamoja na hayo anayotufanyia watanganyika sio sawa,
Inakuaje jamhuri inaongozwa na familia toka zenji