Samia aizika CCM rasmi: Ugonjwa wa mbeleko za kisiasa zaanza kuitafuna CCM yenyewe

Na hio saa haipo mbali,mimi ninachoupendea wakati huwa haudumu , kati ya leo na kesho ni pafupi sana.
Si mbali si siku nyingi. Ukiona siku hiyo watu 5 wanavunjwa miguu lakini watu 200 kati yao wanasonga mbele bila kujali, kuogopa wala kuhofia chochote, na hasira hiyo ikawa Nchi nzima, ujue saa ya ukombozi imefika. Pressure ikiwa kubwa kiasi hicho, hata Askari huungana na Wananchi. Kwa sababu wanakuwa wamepiga risasi na wamechoka wao lakini watu bado wanasonga mbele.
 
Hata kama wangefuata huo utaratibu waliojiwekea unafikiri ni nani anaweza kumpinga rais na mwenyekiti? Kama lowasa hakuweza unafikiri Kuna mtu angethubutu kumpinga Samia?

Rais na mwenyekiti wa ccm ana nguvu kubwa Sana ukitaka kupotea kisiasa jaribu kum challange. Unamkumbuka John shibuda?
 
CCM imeshajifia kitambo ...kinachowasaidia ni majeshi na bunduki zao!!
 
Naona watu mnatokwa na mapovu bure,ccm tuna utaratibu wetu wa kuachiana nafasi ndani ya miaka 10,kwahiyo kwa utaratibu huo bado mama angebakia

Lakini hata kama angejitokeza mtu wa kujaribu kugombea ndani ya chama bado asingepita kutokana kwa utaratibu uliowekwa

Tatu kilichofanyika leo ni kuokoa mda na kuyafanya mambo yasiwe mengi,kikubwa wanachama wameridhika na azimio limepitishwa,je shida iko wapi?

Kitachofuata ni utaratibu tu wa kuchukua form rasmi na kazi iendelee,kwahiyo malalamiko yenu wala hayana mashiko hapa

Lau ingekuwa 2030 ndio mambo yanafanyika mngekuwa na hoja

Ccm oyeeee!
 
Hivi aliyesema mende ameangusha kabati, alimaanisha nn?
 
Unahisi CCM inazikika kirahisi hivyo ?kuna chama cha kuiondoa CCM madarakani?
 
CCM bwana, ilijifanya kama haipo ghafla imekuja na bonge la surprise na Sasa nyumbu wanakanyagana tu; mara waseme hili mara lile
 
Wewe utakuwa ni mwana CCM, na kinachokuuma ni watu wako au wewe kukosa fursa, Huna Nia njema wala na sisi raia; Nasemaje, Nasemaje, Peleka upumbavu wako huko!
 
Ya
Yah upo utaratibu ila Bado mgombea anachukua form na kuzunguka kuomba wadhamini. Ni process lazima ifuatwe. Mkutano mkuu kuamua tu kuimpose kwa kulazimishwa na Kamati kuu tu???
 
Kuna watu wanafarijiana humu wakati hawamjui mwenyekiti na makamu wa chama chao ninani! Ccm wako mbele hatua 100
 
Mimi nimefurahi sana kuona ccm inafanya hivyo, tunaelekea pazuri kweli kweli. Dalili za mvua kunyesha ni mawingu. Mimi naamini 2025 ccm watapoteza viti vingi sana vya wabunge na kushinda urais kwa mizengwe.
Watapoteza viti vingi kama chadema itakuwa chini ya Lisu ila chini ya huyu mlevi ccm itanyakuwa viti vyote....
.. Rejea uchaguzi wa selikali za mitaa
 
Ya

Yah upo utaratibu ila Bado mgombea anachukua form na kuzunguka kuomba wadhamini. Ni process lazima ifuatwe. Mkutano mkuu kuamua tu kuimpose kwa kulazimishwa na Kamati kuu tu???
Unamaanisha nini kusema wamelazimishwa? Wakati umeona vibe la wajumbe liko juu kumtaka Mama Samia aendelee

Au mimi ndio sielewi?
 
This was an outside job na dola zote za kule zilippromoka

You can’t compare na tanzania ambapo mabeberu are benefiting from
The current status

Arab spring was also an outside job

Understand the context

The outsiders have interest in shaping and guiding away Tanzania from the Russo Arabian influence
 
Unamaanisha nini kusema wamelazimishwa? Wakati umeona vibe la wajumbe liko juu kumtaka Mama Samia aendelee

Au mimi ndio sielewi?
Mwenye nguvu akikusimamisha mbele akikuuliza swali ni lazima ulijibu. Kama wamependa kwa nini aliwakemea kampeni za mapema wakati yeye kaanza kabla ya wakati?
 
Hata ile fomu moja Mama kaikimbia?😅😅
 
Ccm ina wenyewe, ccm ni kikoba cha watu ,wao ndo wanajua wanampataje wanae muhitaji kushika kijiti.
 
Mwenye nguvu akikusimamisha mbele akikuuliza swali ni lazima ulijibu. Kama wamependa kwa nini aliwakemea kampeni za mapema wakati yeye kaanza kabla ya wakati?
Mambo ya ngoswe muachie ngoswe mwenyewe expert wangu,imeisha hiyo,samia mitano tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…