SAMIA: Aliyepitia Njia Haramu, Haiwezekani Awe Halali

Mkutano mkuu wa CCM unayo mamlaka na wajibu wa kuanzisha,kuondoa na kufanya maamuzi kuhusu jambo lolote.

Siyo kweli, umesema uwongo. Mkutano mkuu upo kwa mujibu wa katiba, na hauna mamlaka ya kukiuka katiba. Mamlaka ya mkutano mkuu yanaishia kuidhinisha mapendekezo ya mabadiliko ya katiba ya chama yanayokuwa yameletwa na Halmashauri Kuu ya chama. Lakini hauna uwezo wa kuandaa mapendekezo ya mabadiliko ya katiba, halafu tena uidhinishe mapendekezo hayo. Na kamwe mkutano mkuu hauna mamlaka ya kufanya chochote nje ya katiba ya chama, katiba ya nchi au sheria za nchi.
 
Hakuna aliye halali mbele ya macho ya watanzania NO REFORMS NO ELECTION NDIO DAWA PEKEE MENGINE NI UONGO.
 
Wana CCM hatulalamiki ila wavimba macho ndio kutwa kucha kupiga kelele. Si mahakama zipo? Nendeni mkamzuia kama mna hoja na sio kila siku kutupigia kelele.
 
Duh watu wamemkalia kooni kweli kweli,nasema uongo ndugu zangu,msema kweli ni mpenzi wa Mungu
 
Sasa mimi na wewe nani muongo ndugu,tatizo ni kutumia hisia kuliko usahihi. Katiba ya CCM unaijua lakini? Wakati mwingine ni vizuri kuficha mihemko... Katiba ya nchi inasema kupendekeza wagombea ila aijasema kua chama cha Siasa akitapendekeza mwanachama kama Bunge alijavunjwa. Lakini pia,katiba na utamaduni wa CCM nikua mgombea atoshindanishwa pale atakapokua anatafuta next term ILI LIWEKE AKILINI
 
Hata yale yanayovunja katiba ya nchi? Kama ndivyo mkutano mkuu wa ccm upo juu ya katiba ya nchi? Hacheni porojo kwenye mambo ya msingi.
Katiba ya nchi imesema wagombea wa urais nasio wagombea kupitia vyama.. Someni katiba vizuri.
 
Touc
Touchable
 
Mna kazi nzito sana kuweza kuupinga uwezo wa kazi anazofanya Samia nchi nzima.

Mnapopoteza nguvu hapa JF Samia anakamilisha ujenzi wa viwanja vya ndege na kuzinunua nyingine zinazolifanya shirika kuwa la kimataifa.

Mnapojaribu kumtusi humu jukwaani huko mikoani umeme wa REA unakaribia kuifikia nchi nzima kuanzia kule Lindi mpaka Bukoba vijijini panawaka taa na shughuli inabakia kwa wenyeji kuja na ubunifu wa masuala ya kiuzalishaji.

Mnapokuja na siasa za mipasho za kwenye kanga humu jukwaani, huko nje Samia anapeleka boti maalum za kiafya kwa ajili ya wananchi wanaoishi kwenye visiwa vya Ziwa Victoria kwa ajili ya kuokoa uhai wao.

Mnapoendekeza maneno ya chuki humu jukwaani fursa nyingi kwa wakulima zinafunguliwa naa wanaunganishwa na masoko ya mazao yao kule Asia.

Bandari inaendelea kuongeza pato kwenye uchumi wa taifa. Mna kazi kubwa sana ya kufanya kujaribu kuonyesha awamu ya sita haijafanya lolote, hospitali za rufaa zinajengwa na kusogeza huduma kwa wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…