The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 11,099
- 13,709
Kuongoza taifa siyo sawa na kupika au kufua nepi. Kunataka jabali tena mwenye elimu, busara, na akili timamu.
Tanzania, tumejaliwa kila kitu ila huyo hapo juu. Uongo umegeuzwa uongozi. Upigaji dili umegeuzwa maadili. Ndiyo maana tunapata watawala wa hovyo kama hawa. Kweli CCM mmejua kututenda. Mmetuua na kutuita wageni.
Kama kweli wageni ndiyo walifanya maandamano, mnataka kujadiliana na nani? Mbona hatuonyeshwi hao wageni na kutajiwa majina yao. Kama kuna wageni, basi waliosababisha 'wageni' kufanya maandamano, ndiyo wageni.
Kama waliofanya maandamano si watanzannia, sijui waliowachochea kwa ubinafsi, ufisi, ufisadi, na uchafu mwingine tuwaiteje? Ni vibaya sana kujidanganya halafu ukawadanganya na wengine nawe ukiwamo. Gen Z siyo kizazi cha Nyerere wala Karume.
Wamesoma na wanaelewa mambo. Wana mtandao kama silaha yao. Ukiwaua, huwezi kuficha uzandiki wako.
Nawahimiza CHADEMA wasikubali kugeuzwa taulo la kufutia damu ya Samia. Kama majadiliano, wakajadiliana na yule mgeni toka DRC, Zitto Kabwa na mwenzake Hashim Rungwembwa.